MWANASHERIA MAARUFU JIJINI ARUSHA ASHIKILIWA NA POLISI
JESHI la polisi mkoani Arusha linamshikilia na kumhoji mwanasheria maarufu jijini hapa,Deogratias
Urasa kwa tuhuma za kufyatua risasi hovyo katika ugomvi baina yake na
mfanyabiashara maarufu,James Ndika anayeishi
jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na kamanda mkuu wa
jeshi la polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabas alisema kwamba tukio hilo
lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika mgahawa maarufu wa ViaVia uliopo
mkabala na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Mgahawa wa Viavia umejijengea umaarufu kwa kutembelewa na raia
wa wageni kutoka nchi za Ulaya,Marekani na Asia ambapo katika siku za hivi
karibuni umekumbwa na matukio ya watu kupigana hovyo.
Kamanda,Sabas alisema kwamba pamoja
na mwanasheria huyo
anayefanya kazi kutoka kampuni ya Maro Advocates ya jijini Arusha
kufyatua risasi tatu hovyo hewani lakini katika tukio hilo hakuna mtu
yoyote
aliyejeruhiwa.
Alitaja chanzo cha ugomvi katika tukio hilo ni baada ya
kutokea majibishano makali baina ya mwanasheria huyo na Ndika yaliyosababishwa na masuala ya kibiashara miongoni mwao.
“Hawa watu wana mambo yao ya kibiashara sasa siku ya tukio walijibishana
ndipo huyu mwanasheria akachukua silaha yake na kufyatua risasi hewani hovyo
hali iliyopelekea kuleta taharuki”alisema Sabas
Alisema kwamba mara baada ya majibishano hayo mwansheria
huyo alikosa uvumilivu na kufyatua risasi hewani hali iliyopelekea taharuki ndani ya mgahawa huo na kupelekea watu kukimbia
hovyo huku wengine wakilala chini kuhofia usalama wa maisha yao.
Kamanda,Sabas aliliambia gazeti hili
kwamba baada ya jeshi lake kupokea taarifa lilimshikilia mwanasheria
huyo katika kituo kikuu cha polisi cha kati na kisha kumwachia huru
ambapo kwa sasa yuko nje kwa dhamana.
Alienda mbali na kusisitiza ya kwamba mbali na kushikiliwa jeshi lake lilimhoji mwanasheria huyo juzi atika makao
makuu ya jeshi hilo mkoani hapa na pindi uchunguzi utakapokamilika atafikishwa
mahakamani kujibu makosa yanayomkabili.
Alisisitiza
kwamba mbali na kushikiliwa kwa mwanasheria huyo pia jeshi lake
linawasaka watuhumiwa wawili(majina yao yamehifadhiwa) wanaotajwa
kuhusika kwa ukaribu katika tukio hilo .
Habari hii imeandikwa na mosses mashala ,Arusha
Habari hii imeandikwa na mosses mashala ,Arusha
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia