Wito
umetolewa kwa serekali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuakikisha
kuwa inaboresha mazingira ya Afya ili kuwezesha madktari kuweza kufanya
kazi zao kiufanisi na kuokoa maisha zaidi.
Wito huo umetolewa na Katibu Rasilimali watu kutoka Sekretariet ya jiji la Arusha Bwana Mwanga Exaud wakati akifungua mkutano wa Nane (8) wa madactari wanafunzi kutoka nchi za afrika zipatazo 310 katika ukumbi wa mikutano hotel ya ngurdoto jijini arusha.
Alisema kuwa mkutano huo wanafunzi hao udaktari wamekutana katika mkutano huo katikaa kujadili maswala mbali mbali yanayo kabiliana nayo katika sekta hiyo ya katika nchi za afrika ni lengo zuri la kua na wataalam wa afya wenye malengo na taaluma hiyo.
‘’lengo
kubwa la mkutano huo ambapo Tanzania ambao ni wenyeji ni kuwakutanisha
wanafunzi hawa wa Udokta barani afrika ili kujadiliana nao changamoto
mbalimbali wanazokabiliana nazo katika nchi zao katika sekta ya afya”,
Alisema Bwana Exaud.
Aidha aliongezea kusema kuwa katika mkutano huo ambao awali walianza kwa semina za awali
za maswala mbali mbali ya afya likiwemo swala la muongozi pomoja na
maswala mbalimbali yahusianayo na sekta ya afya huku baada ya ufunguzi
huo ndani ya siku tano watajadili changamoto mbalimbali.
Pamoja na hayo alisema kuwa kutokana kuwepo na changamoto nyingi ndani ya sekta hiyo ya afya yeye anaona
kuwa kuna umuhimu mkubwa wa madaktari hao wanafunzi kukaa kwa pamoja
ambapo hii itasaidi kuondoa migogoro ya madokta kugomea wagojwa na
kupelekea kifo.
Manga amewataka madactari
hao wanafunzi kutumia vyema mkutano huo wa siku tano kuakikisha
wanafikia kauli mbiu ya kutatua migogoro katika sector ya afya
nakuadhimia malengo ya pamoja yenye nia ya kujenga sector za afya barani
afrika.
Kwa
upande wake rais wa jumuiya hiyo ya wanafunzi madactari kutoka nchi za
afrika bwana Frances Tegete ameeleza kuwa mkutano huo pamoja na
kuangazia maswala ya changamoto pia wamelenga kuelimishana namna ya kufanya utafiti wa madawa feki yanayotumika katika jamii.
“
Mkutano huo utalenga mambo muhimu ikiwemo rasilimali watu vitendea kazi
vya afya pamoja na uwajibikaji wa kitaalamu katika sector ya afya
barani afrika na kila mwakilishi wa nchi yake atapata fursa ya kuchangia
maswala haya muhimu”, Alisema Bwana Tegete .
mwenyekiti
wa mkutano huo bwana Florence mwitar alisema kuwa Tanzania imebaatika
kuandaa mkutano huo ambao ulalengo la kutatua migogoro hilioko katika
sector ya afya barani afrika ambapo wanafunzi madacrari watazungumzia
migogoro hiyo kwa undani .
mkutano huo utalenga katika rasili mali watu katika sector ya afya pamoja na miundo mbinu ya afya kuboreshwa na kuwa ya kisasa kwa nchi za afrika kuenenda na wakati wa kutumia vifaa vya kitaalamu zaidi na kuondokana na changamoto katika sector ya afya inayo ikabili kwa sasa
Mwenyekiti
Florence ameiyomba serikali kuunga mkono umoja wa madactari wanafunzi
kuendelea kufanya mikutano ya pamoja kwa kuchangia garama za kuandaa
mikutano ya kila mwaka nasio kuachia tu vyama vya wanafunzi wa vyuo vya
madactari kuanda peke yao kwani ni gharama kubwa .
MWISHO
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia