msanii huyo akitafakari kwa kina mara baada ya kuanguka chini ya jukwaa huku wenzake wakimpa pole
msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikwa na wasanii wenzake
mara baada ya kuanguka jukwaani juzi ndani ya uwanja wa Sheikh Amri
katika tamasha la wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wale wa filamu.
.msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikiliwa na wenzake
wakimshusha chini ya jukwaa mara baada ya kuanguka alipopewa nafai ya
kuwasalimia mashabiki wake
HALI ya
msanii wa filamu nchini,Juma Said
Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka
jukwaani mara baada ya kuishiwa na nguvu wakati alipopewa kipaza sauti
kuwasalimia mashabiki waliofurika kumtizama.
Tukio hilo
lilitokea juzi jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki
wa kizazi kipya lililofanyika ndani ya
uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid
wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.
Mara baada
ya msanii huyo kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia
mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu”ahhh"
na kisha kudondoka chini ya jukwaa lakini kabla ya kutua chini alidakwa na wasanii
waliokuwa pembeni yake.
Hatahivyo,wasanii
hao walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya
muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa kupumzika
zaidi.
Akihojiwa na
gazeti hili muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole
alisema kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji
matibabu zaidi.
”Kaka hali
yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”alisema Sajuki huku
akionekana mnyonge zaidi
Hatahivyo,baadhi
ya mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali
ya msanii huyo huku wengine wakiwatupia lawama nzito baadhi ya wasanii wa
filamu nchini walioambatana na msanii huyo kwa madai kwamba wanamtumia ili
wapate pesa ihali mwenzao ni mgonjwa.
Wakihojiwa
kwa nyakati tofauti mashabiki hao kwa jazba walisema kwamba msanii huyo alipaswa
kupewa muda mwingi wa kupumzika kuliko kuambatana na wenzake mikoani kwani hali
hiyo inamchosha zaidi.
“Hawa watu
wa Bongo movie ni watu wa ajabu sana huyu mtu anaumwa sana sisi tunashangaa
wanaambatana na mtu mgonjwa mikoani wampe muda apumzike na si kumtumia kwa
kupata pesa”alisikika shabiki mmoja akiongea kwa jazba