KESI YA MWISHO ICTR DHIDI YA WAZIRI WA ZAMANI KUTOLEWA HUKUMU DESEMBA 20
Arusha,
Desemba 1,2012 (FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya
Rwanda(ICTR) itatoa hukumu ya kesi inayomkabili Waziri wa zamani wa
Mipango wa Rwanda,Augustin Ngirabatwara Desemba 20, 2012, kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na Mahakama hiyo.
Hii itakuwa na kesi ya mwisho kutolewa hukumu na mahakama hiyo ya awali ya Umoja wa Mataifa.
Iwapo
kutakuwapo na kukata rufaa baada ya hukumu, rufaa hiyo itasikilizwa na
Taasisi Itakayorithi Kazi za Mahakama Mbili za Umoja wa Mataifa (MICT)
ikiwemo ICTR na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita Katika
Yugoslavia ya zamani (ICTY).
Wakati
wa kuwasilisha hoja za mwisho Julai 23, mwaka huu, mwendesha Mashitaka
aliiomba mahakama hiyo kumpatia adhabu ya kifungo cha maisha jela Waziri
huyo iwapo atatiwa hatiani kwa kuhusika na mauaji hayo mwaka 1994.
Akitoa
sababu kwa nini Waziri huyo apewe adhabu kali kiasi hicho, Mwendesha
Mashitaka, Rashid Rashid alisema ‘’kutokana na ushahidi ulitolewa
mahakamani, nia ya Ngirabatware ya kutekeleza mauaji ya kimbari
imethibitishwa pasipo mashaka.’’
‘’Alitekeleza,
kuandaa,kuchochea, kuhimiza, kusaidia na kupitisha adhma ya mauaji
dhidi ya raia wa Kitutsi.Ametekeleza uhalifu huo katika wilaya
alikozaliwa ya Nyamyumba, mkoa wa Gisenyi, Kaskazini mwa Rwanda,’’
mwendesha mashitaka alisema.
Kwa
upande wake, Wakili wa utetezi katika kesi hiyo , Mylene Dimitri
aliiomba mahakama iliyokuwa inaongozwa na Jaji William Sekule toka
Tanzania,imwachie huru mteja wake kwa madai kwamba mwendesha mashitaka
ameshindwa kuthibitisha mashitaka pasipo mashaka.
‘’Ushahidi
uliotolewa na Ngirabatware ni zaidi ya ushahidi wa kuaminika na
umeonyesha zaidi ya vigezi vya kuwepo mashaka katika kesi ya mwendesha
mashitaka hivyo hamna budi kumwachia huru,’’ Wakili Dimitri aliisihi
mahakama.
Alisema
mteja wake kamwe hakushiriki katika mauaji dhidi ya Watutsi na kwamba
ushahidi wa utetezi uliotolewa katika kesi hiyo ulikuwa ‘’ wenye maana,
haikuegemea upande wowote na wa kuaminika kwa kiwango cha hali ya
juu,’’
Wakati
wa usikilizaji wa kesi yake, Ngirabatware alitoa sababu kadhaa ikiwa ni
pamoja na kwamba hakuwapo nyumbani kwao wakati uhalifu ulipokuwa
unafanyika. Alidai kwamba kati ya Aprili 23 na Mei 23, 1994, alikuwa
katika safari za kikazi katika nchi mbalimbali zikiwemo, Senegal, Gabon
na Uswisi.
Lakini
mwendesha mashitaka alipingana na ushahidi huo kwa kudai kuwa katika
kipindi hicho, mshitakiwa alikuwa mkoani Gisenyi, hususan ni katika
wilaya yake ya Nyamyumba kushiriki katika kutenda uhalifu huo.
Waziri
huyo wa zamani anashitakiwa kwa kula njama za kufanya mauaji ya
kimbari, mauaji ya kimbari au kushiriki mauaji hayo, uchochezi,
kuteketeza kizazi na ubakaji kama uhalifu dhidi ya binadamu.
Na Nicodemus Ikonko, Hirondelle, Arusha
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia