BREAKING NEWS

Monday, December 24, 2012

MAELFU YA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA WAJITOKEZA KUMPOKEA MBUNGE LEMA.


DSCF3646
KAMANDA MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA AKIWASALIMIA WANANCHI WA ARUSHA BAADA YA KUWASILI KUTOKEA DAR ES SALAAM ALIPOSHINDA RUFAA YAKE YA KUPINGA KUVULIWA UBUNGE WAKE.
HOI-HOI na nderemo zilisikika zikiandamana na msongamano wa watu warika mbalimbali  jijini Arusha siku ya Jumamosi 22, 2012 wakati wakazi wa jiji hilo walipo jitokeza kumlaki mbunge wao wa Arusha mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema Kamanda Godbless Lema mara baada ya kuwasili kutokea Dar es salaam ikiwa ni siku moja tu kufwatia ushindi wake wa rufaa ya kupinga kuvuliwa ubunge wake.

Jiji la Arusha lilipambwa na rangi za chama cha CHADEMA huku shamrashara za aina yake zikitanda ndani ya jiji hilo, sauti za wananchi zilisikika zikiimba nyimbo za ukombozi na kumtaja Kamanda Lema kama shujaa, magari, pikipiki na watu walionekana wakiwa wamebeba bendera, matawi pamoja na mabango yaliokuwa na ujumbe mbalimbali.

Tukio hilo ambalo  lilikuwa la aina yake liliwashirikisha pia viongozi mbalimbali wa chadema waliomsindikiza Kamanda Lema kwa maandamano yaliyoanzia uwanja wa  ndege wa kimataifa(KIA) mpaka jijini Arusha.

Kamanda Lema alipopata nafasi ya kuongea na wananchi wakazi wa Arusha katika uwanja wa Ngarenaro aliuwaambia umati huo kuwa moja ya kazi ya mbunge ni kuwapigania watu na si vinginevyo hivyo wasiwe na hofu mtetezi wao amerudi na waliomshtaki watalazimika kumlipa fidia.

Aliongeza kwa kusema kuwa  toka wananchi wamchague kuwa mbunge, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipanga mikakati ya kumchafua lakini kwa msaada wa Mungu na wananchi wenye mapenzi mema ameweka historia katika Nchi hii ya Tanzania.

“Toka niwe mbunge nimekuwa mbunge wa misukosuko kwa sababu nakataa wanachi wangu wasionewe hovyo na pia nawafundisha ujasiri, msikubali kuonewa” alisema Lema

Kwaupande wake Mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki Kamanda Jushua Nassari alisema kuwa Bunge lijalo watapeleka hoja nzito zenye lengo la kuwakomboa watanzania.

“Leo namkabidhi Lema fimbo yake ya ubunge aliyonikabidhi mara baada ya ubunge wake kutenguliwa, aliponiachia jimbo aliniambia niwapiganie watu kwahiyo nilazima nimpe ripoti ya jimbo ili ajue pa kuanzia”alisema Nassari

Mh.Nassari akisoma ripoti kwa Mbunge Lema huku akiushambulia mradi wa ujenzi wa barabara unaoendelea jjijini Arusha akibainisha kuwa haukidhi viwango kwa kuwa ujenzi huo unajengwa kiholele tena kwa mwendo wa taratibu

“Nashangaa kweli huu mradi hata sehemu za watu kuegesha magari hakuna na pia sehemu ya watembea kwa miguu ni mkandarasi gani au kongozi yupi aliye ruhusu ujenzi huu”? alisema Nassari

LEMA WATU ARUSHA
KAMANDA LEMA AKIWA PAMOJA NA VIONGOZI WA CHADEMA KWENYE GARI LA WAZI BAADA YA KUPITA SANAWALI KWENYE MATAA , HUKU WANANCHI WAKIWA WANALISIDIKIZA ALIPOKUWA ANAWASILI JIJINI ARUSHA AKITOKEA DAR ES SALAAM ALIPOSHINDA RUFAA YA KESI YAKE YA KUPINGA KUVULIWA UBUNGE.
LEMA MNARA WA SAA
KAMANDA LEMA AKIWA PAMOJA NA VIONGOZI WA CHADEMA KWENYE GARI LA WAZI BAADA YA KUPITA MNARA WA SAA KATIKATI YA JIJI LA ARUSHA , HUKU BODA BODA NA MSAFARA WA MAGARI PAMOJA NA WANANCHI WATEMBEA KWA MIGUU WAKIWA WANALISIDIKIZA ALIPOKUWA ANAWASILI JIJINI ARUSHA AKITOKEA DAR ES SALAAM ALIPOSHINDA RUFAA YA KESI YAKE YA KUPINGA KUVULIWA UBUNGE.
LEMA AKIPUNGIA(1)
KAMANDA LEMA AKIWA PAMOJA NA VIONGOZI WA CHADEMA KWENYE GARI LA WAZI BAADA YA KUPITA SANAWALI KWENYE MATAA , HUKU WANANCHI WAKIWA WANALISIDIKIZA ALIPOKUWA ANAWASILI JIJINI ARUSHA AKITOKEA DAR ES SALAAM ALIPOSHINDA RUFAA YA KESI YAKE YA KUPINGA KUVULIWA UBUNGE.
DSCF3578
MSAFARA WA KAMANDA LEMA ULIONGOZWA NA BODA BODA AMBAZO ZILITANGULIA ALIPOKUWA ANAWASILI JIJINI ARUSHA AKITOKEA DAR ES SALAAM ALIPOSHINDA RUFAA YA KESI YAKE YA KUPINGA KUVULIWA UBUNGE.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates