UMOJA
wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoani Arusha umesema haupo tayari
kukiachia chama chochote cha upinzani kuongoza dola kwakua vyenyewe wala
viongozi wake hawajui maana ya dola.
Aidha
alisema katibu mkuu wa Chadema Dk.Wilbroad Slaa ni popo kwakua anamiliki kadi
za vyama viwili vya CCM na Chadema hali inayoonyesha kuendelea kukipenda CCM na
kwamba ni kiongozi asiye na masimamo na hafai kuongoza.
Kauli
hiyo imetolewa jana na mwenyekiti wa UVCCM mkoa huo Robson Meitinyiku alipokua
akizungumza katika kikao cha baraza maalumu la jumuiya hiyo ambapo kilikua na
agenda kuu ya mbili za kuchagua kamati yake ya utekelezaji pamoja na uteuzi wa
katibu hamasa wake.
Meitinyiku
alisema kwa kauli moja jumuiya yake imekubaliana hivyo kutokana na kujiridhisha
kuwa hakuna kiongozi wala chama cha upinzani kinachojua maana ya dola kutokana
na vitendo vyao mbalimbali vya vurugu,kashfa kwa uongozi wa serikali pamoja na
kwa vyombo vyote vya dola.
Alisema
katika kuhakikisha hayo yanafaniki katika baraza hilo wanawekeana mkakati watakaokubaliana kwa
pamoja kwa vijana hao kuwa wamoja na kuachana na makundi na kuwashughulikia
wale wote watakaokiuka makubaliano hayo.
Alisema
anatambua fika kuwa vyama vya upinzani vimekuwa vikitumia mipasuko
inayojitokeza katika chama chao hususani jumuiya hiyo ya vijana ambayo ndiyo
jeshi la chama chake kitu kinachosababisha mipasuko na kuyumba kwa chama.
“sisi
ni vijana naamini kwasasa ni wamoja na umoja siku zote ndiyo ushindi sasa mwenyekiti wa chama
nakuahidi tutalirejesha jimbo letu la Arusha lililokua mikononi mwa mbunge wa
Chadema”alisema Meitinyiku.
Alisema
yeye kama vijana na jumuiya yake hatokubali kuona mji wa Arusha ukiendelea
kuyumba kiuchumi kutokana na vurugu zinazofanywa na viongozi wa Chadema akiwemo
aliyekua mbunge wa jimbo la Arusha Godbles Lema ambapo pia uliathiri kwa kiasi
kikubwa uchumi wa vijana wanaoanza maisha.
Katika
kikao hicho wajumbe wa watano walichaguliwa kuunda kamati ya utekelezaji ambapo
kwa wilaya ya Arusha alichaguliwa Amina Msangi,KaratuJackob Doday,wilaya ya
Meru Titto Nassari,Arumeru Noel Severe na Monduli Diwani Kimey huku katika
nafasi ya katibu hamasa alichaguliwa kwa mara nyingine mtoto wa mbunge wa
Monduli Edward Lowassa,Fred Lowassa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia