watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamekamatwa na wananchi baada ya kuwashika wakijaribu kutorosha zaidi ya mita 500 za yaya za shaba walizokata kwenye laini ya umeme ya Usa feeder iliyopo wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Akizungumzia kutoea kwa tukio hilo tukio meneja wa Tanesco mkoa Engineer Nicholaus Kamoleka alisema kuwa tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki eneo la Kikatiti Wilaya ya Arumeru, kwa Mangasha.
Adha alibainisha kuwa siku ya tukio watu hao walikamatwa na Wananchi wenye hasira kali kwa kushiriana wafanyakazi watanesco na walikamatwa kuwa ni pamoja na William Jonas (20), Hussein Abubakar (19), na Luwaich August (23) wote wakazi wa Daraja mbili Unga Ltd.
Aidha alibainisha kuwa baada ya umeme kukatika saa 8.30 usiku, ushirikiano kati ya wafanyakazi wa kituo cha TANESCO Usa river na viongozi wa kijiji cha Kwa mangasha ndio uliweza kuwasiliana na kufuatilia swala hili ndipo walipowakuta watuhumiwa hawa na kukamatwa.
Kamoleka alisema kuwa tukio hilo la wizi limesababisha Tanesco hasara ya Shilingi Millioni Ishirini na liliathiri mikoa miwili,mbapo alibainisha kuwa wateja wa Wilaya nzima ya Arumeru Mkoani Arusha na pia Wilaya nzima ya Hai mkoani Kilimanjaro walikaa bila umeme kwa masaa 12, kuanzia saa nane usiku hadi saa nane mchana.
Alisemakuwa Watuhumiwa hao wako chini ya ulinzi wa Polisi na uchunguzi unaendelea huku akibainisha kuwa Baada ya matukio ya wizi wa nyaya za shaba kuwa mengi katika laini ya umeme kubwa ya Usa river,Idara ya Usalama ya TANESCO Arusha ulimeanza kuzunguka na kuelimisha wananchi wa maeneo umeme unapopita na vijiji vya karibu kuwa ni jukumu lao katika kulinda miundo mbinu, pia imeanzisha mfumo wa ulinzi shirikishi ambao umesha fanikisha kukamatwa watuhumiwa wanne hadi sasa.
Kamoleka aliwataka wananchi wa mkoa mzima wa arusha kuwa makini na kuendelea kutoa ushirikiano kwa tanesco kwa kuwafichua watu wote ambao wamekuwa wanafanya kazi yakuina nyaya za shaba pamoja na kuwafichua vishoka wote na wale watu ambao wamejiunganishia umeme bila kufuata utaratibu wa tanesco