MSAADA ZAIDI UNAHITAJIKA KURUDISHA HALI YA BI ARAFA BAADA YA KUFIKISHWA MUHIMBILI HOSPITAL
Pichani....Bi Arafa akiwa na Msamalia mwema anaemsaidia kuhakikisha
hali ya Mgonjwa huyo Inaimarika
Bi Arafa Issa akiwa katika kitanda cha ward namba 20 Sewa
Haji-Muhimbili hosp asubuhi ya leo
Bi Arafa Issa mwenye umri wa Miaka 38 mkazi wa Kijiji cha Narung'ombe
wilayani Ruangwa ambae anasumbuliwa na Uvimbe baada ya kuumwa Kichwa
na baadae kupata kipele kilichosababisha Uvimbe kama anavyoonekana
Pichani, alifikishwa katika Hospital ya Muhimbili baada ya Wasamaria
wema walioguswa na hali hiyo pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi kujitoa kumsaidia
kumsafirisha toka Kijijini kwao hadi Muhimbili Hospital
Baada ya kufikishwa na kupokelewa amelazwa Block la Sewa Haji Ward na
20 NA Baadae alitakiwa kupimwa kipimo cha CT Scan kufuatia kipimo
hicho Wauguzi wake waliambiwa kipimo hicho kina tatizo na kuelekezwa
kwenda Regency Hospital kupima hali iliyokuwa ngumu kwao kutokana na
gharama kubwa kwao ya kumudu kipimo hichoTshs(264,000/-)
Kwa msaada mwingine Wadau walifanikisha kupimwa kwa mgonjwa huyo na
kupatiwa majibu ambayo yanaelekeza kufanyiwa Upasuaji..
Asubuhi ya Leo nilifika katika hospital hiyo na kuonana na Bi Arafa
ambae analalamika sana kupata maumizi makubwa Kichwa na kudai kuwa
toka amepokewa katika hospital hiyo na kulazwa tarehe 20 NOV 2012 hadi
leo ajapata dawa ya aina yoyote zaidi ya panadol anazonunua hali
inapomzidi
Nilifanikiwa kuwasiliana na muuguzi aliekuwepo zamu asb na baada ya
kupitia file lake alinikabidhi fomu inayoonyesha mgonjwa anatakiwa
apime kipimo kinaitwa MRI Brains na kuelekeza sehemu ya kwenda kulipia
kipimo hicho...Baada ya kuwasilisha hiyo fomu imeatakiwa Tshs Laki
mbili(200,000)Pia itahitajika gharama ya Operesheni ambayo haikutajwa
Kwa niaba ya Bi Arafa Nawaomba wadau mbalimbali ndugu na jamaa
kusaidia hatua inayofuata kumsadia mgonjwa huyo..Yupo hapo Hospital
Unaweza kusaidia kwa njia moja au nyingine
Kwa Mawasiliano zaidi ya mgonjwa huyo wasiliana nami kwa 0716
483532,,,,0787176221 au 0716483532 Abdulaziz Ahmeid wa Lindi Press
Club au abdulaziz762@gmail.com
Nawashukuru wote walioguswa kumsaidia Mgonjwa huyo hadi ilipofikia leo,,Ameen
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia