SASA NI WAKATI WA KUANZISHA SHULE ZA MICHEZO - MH. LOWASSA
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa pili kushoto) akijumuika pamoja na Baadhi ya Wabunge wanaounda timu ya Bunge Sports inayoundwa na wabunge kutoka Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamhuri,wakati wa Chakula cha Mchana alichowaandalia Nyumbani kwake,Ngarashi Wilayani Monduli jana.Wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Mh. Amos Makalla,Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Mh. Iddi Azzan pamoja na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Monduli, Reuben ole Kunai.
Wabunge wanaounda timu ya Bunge Sports inayoundwa na wabunge kutoka Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamhuri wakipata Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Wabunge
wanaounda timu ya Bunge Sports inayoundwa na wabunge kutoka Baraza la
Wawakilishi na Bunge la Jamhuri wakipata Chakula cha Mchana
kilichoandaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh.
Edward Lowassa Nyumbani kwake,Ngarashi Wilayani Monduli jana.Mh.
Lowassa alikutana na Wabunge hao ili kujadili maswala mbali mbali
yahusuyo Michezo hapa nchin,wakati timu hiyo ikiwa Kambini jijini
Arusha,kujiandaa kwenye Jijini Nairobi kwenye Mashindano ya Afrika
Mashariki.
WAZIRI
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa amewashauri
wabunge wa timu ya Bunge Sports kufikiri juu ya kutunga sera ya michezo
itakayoruhusu kuanzishwa kwa Shule za Michezo (Sports Academy) hapa
nchini.
Lowassa
ameyasema hayo jana,baada ya kuialika nyumbani kwake timu hiyo
iliyopiga kambi ya jijini Arusha tayari kwa mashindano ya Mabunge ya
Afrika Mashariki jijini Nairobi.
“Nilisikitika
kweli Timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars ilipofungwa na Burundi kwenye
mchezo wa pili wa Mashindano ya CECAFA huni Uganda, pamoja na juhudi za
Rais Jakaya Kikwete kuleta makocha bado tumefungwa na Burundi iliyotoka
kwenye vita juzi!.
“Nyinyi
ni watunga Sera, ni wachezaji mnajua changamoto zinazofanya tusifike
juu, umefika wakati wa kuwa na Shule za Michezo zinazotambuliwa na Sera
zetu.
“Mpira
ni chakula cha Watanzania, wanapenda mpira sana. Napendekeza baada ya
kurejea anzeni kufikiria juu ya kutunga Sera ya kuwa na Shule za
Michezo. Kipingu amejitahidi kuwa na kitu kama hiki lakini amebakia peke
yake hakuna anayemuunga mkono,” alisema Lowassa.
Alisema
kuwapo kwa Timu ya Bunge Sports kutasaidia kufikiria juu ya mafanikio
ya mchezo wa mpira wa miguu, pete na michezo mingine.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Amos
Makalla aliyeongozana na timu hiyo alimwambia Mh. Lowassa kwamba
serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha Sera za michezo.
“Sera na sheria za sasa za michezo kweli haziendani kabisa na wakat,zote ni za zamani. Serikali imejipanga kuzifanyia kazi.
“Changamoto uliyoitoa ya kuanzisha Shule za Michezo na kuendeleza michezo nchini tunaipokea na tutaifanyia kazi.
“Nilipoteuliwa
kuwa Naibu Waziri kwenye Wizara hii niliwaambia watu na binafsi
namshukuru Rais Kikwete, kwamba upele ulipata mkunaji kwani mimi ni
mwanamichezo na uwanjani ni kiungo mchezeshaji,” alisema Makala.
Naye
Mwenyekiti wa Timu hiyo ya Bunge Sports inayoundwa na wabunge kutoka
Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamhuri, Iddi Azan alimshukuru Mh.
Lowassa kwa mawazo yake na kuahidi kuyafanyia kazi.
“Kwanza
tunaahidi ushindi kwa nchi, Bunge letu na haya uliyoyasema tunaahidi
kuendelea kuyafanyia kazi kwani tunatambua sheria na Sera za michezo
zimepitwa na wakati,” alisema Azan.
Timu
hiyo ya Bunge Sports ilikuwa na wachezaji wake wote waliopo kwenye
kambi jijini Arusha wanaounda timu ya Mpira wa miguu na Pete.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia