BREAKING NEWS

Friday, December 21, 2012

FURAHA ZATANDA KATIKA MITAA YA JIJI LA ARUSHA KUFUATIA LEMA KUREJESHEWA UBUNGE


 wengine walibebana kwenye pikipiki yote hayo kushangilia ushindi wa mbunge wao lema
 katika maeneo ya posta pia vijana walionekana makundi makundi wakiimba na kucheza mara baada ya kupata taarifa kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless lema amerejeshewa ubunge wake
 wananchi wengine walijikusanya kwenye matawi wakawa wanacheza na kushangilia ushindi huo wa rufaa ya lema
vijana wa chadema wakiwa wamepnda kwenye gari aina ya hiece wakishangilia ushindi wa lema


Wanachi wa mkoa wa Arusha leo wamebujikwa na furahaa mara baada ya kusikia kuwa aliyekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Amerudishiwa mbunge wake.

Wakiongea wakiwa na furaha  kwa nyakati tofauti wamedai kuwa wanamshukuru mungu sana kwa kuweza kuwasimamia na kuweza kumuongoza jaji  kuweza kufanya maamuzi mazuri kwa kufuata sheria bila ya kushawishiwa na mtu yeyote.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Omari Ally alisema kuwa godbless Lema anastaili kupewa ubunge wake kwakuwa alichaguliwa na wananchi  wake na sio alitumia njia za uchochoroni.

"unajua kuwa kweli walimuaonea Lema sana kwani alikuwa na anastaili kuwa mbunge wetu  kwani tulimchagua wenyewe na katika wabunge ambao walichaguliwa na kupita kwa kishindo kikubwa ukiangalia  mkoa wa Arusha ni mbunge huyu wa Arusha mjini pamoja na mbunge wa jimbo la Arumeru hivyo jamani mungu  katenda miujiza kweli tulianza na mungu na tutamaliza na mungu"alisema Mathayo mushi


Naye mwananchi mwingine ambaye alijitambulisha kwa jina la Neema Raphali alisema kuwa yeye anapenda kumuomba mbunge huyu kuanza kazi kwa kuwatetea wamama ambao wanauza mboga pamoja na nyanya na matunda wakiwa wamebeba katika makarai yao kwani wamekuwa wananyanyaswa sana kwa kunyanganywa vitu vyao hivyo alimuomba mbunge lema kuanza na kuwatetea wao kwani wameteseka kwa muda mrefu.

 Nipashe ilishuhudia wamachinga mbalimbali walikuokuwa wameweka vitu vyao barabarani wakifurahia kwa shangwe huku wakibainisha kuwa mtetezi wao amekuja na kwa sasa watafanya biashara bila ya kubuguziwa na mtu yeyote kwani atawatetea.

"kwakweli tunafuraha ambayo atuwezi kuelezea mtetezi wetu amekuja bwana na uhakikia izishida za kufukuzwa zitaisha na  kweli sasa ivi mgambo yeyote aote kuja kutunyanganya kitu au amnyanganye mama yeyote atatutambua "walisema wamachinga hao


Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates