BREAKING NEWS

Saturday, December 15, 2012

CCM YAELEZA MBINU CHAFU ZA CHADEMA DARAJA MBILI

 mmoja wa wahudumu wa hospitali ya mkoa ya Mounti Meru akiwapa maelekezo viongozi wa chama cha mapinduzi  pamoja na wanachama wa UVCCM waliotembelea hospitali hiyo kwa ajili yakutoa misaada kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapa wa kwanza kulia ni Katibu wa UVCCM mkoa wa Arusha Salus Kidima akifuatiwa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa Robson Meitinyiku
 mjumbe wa baraza kuu  la UVCCM taifa toka mkoa wa Arusha Benson Mollel  wa kwanza kushoto akifuatiwa na mwenyekiti UVCCM mkoa Robson Meitinyiku wakiwa wanatoa msaada kwa mtoto Frank aliyekuwa amelazwa hospitali ya mounti meru
 Mwenyekiti wa UVCCM Robson Meithinyiku akiwa anapeleka msaada kwa wamama waliokuwa wamelazwa wodini
Picha juu na chini ni  wajumbe wa UVCCM pia walikuwepo katika swala zima la kugawa  misaada kwa wagonjwa walikuwa wamelazwa katika hospitali ya mounti meru

 Mwenyekiti akimfariji mtoto mara baada ya kumkabidhi msaada

 Viongozi wa chama cha mapinduzi  wakiwa wanaimba wimbo wa chama kabla ya mkutano wa baraza la uvvccm mkoa wa Arusha
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo Nangole akiwa anazindua rasmi mkutano wa baraza la UVCCM uliofanyika katika hotel ya golden rose mkoani Arusha ambapo katika mkutano huo walizungumzia mambo mengi ikiwemo  kuondoa makundi yaliopo katika chama chao na kujipanga kikamilifu katika kuimarisha chama chao


wajumbe walikuwa makini kusikiliza nini haswa kinazungumzwa
CHAMA Cha Mapinduzi kimesema chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)mkoani Arusha kilitumia mbinu chafu kushinda katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya daraja mbili jijini Arusha.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo Nangole alitaja moja ya mbinu hizo kuwa ni kuwashawishi wafuasi wake kupiga kura mapema na kasha kuanzisha fujo ili kuwatisha wanawake na wazee kutojitokeza kupiga kura.
Aliyasema hayo jana alipokua akifungua kikao cha baraza maalumu la UVCCM mkoani hapo ambacho mbali na ajenda zingine kilichagua wajumbe wa kamati ya utekelezaji na katibu hamasa wake.
Alisema kutokana na vurugu hizo walizokua wakifanyiwa watu wa makundi hayo pindi walipokua wakitoka majumbani mwao kwenda katika vituo vya kupigia kura vilisababisha wengi wao kurudi majumbani mwao kwa kuhofia usalama wao.
Alisema baadhi ya watu wa makundi hayo waliofanikiwa kupiga kura walilazimika kusindikizwa na vijana wa CCM kwenda vituo vya kupigia kura lakini wengi walishindwa kutokana na kuchelewa kugundulika kwa mbinu hiyo chafu kwa vyombo vya dola likiwemo jeshi la polisi.
Kufuatia vitendo hivyo Nangole aliwataka vijana hao kupitia jumuiya yao hiyo kujibu mapigo hayo dhidi ya vitendo hivyo vichafu kwa wao nao kujitokeza kwenda kupiga kura mapema ili kupambana na wafuasi na vijana wa Chadema pindi kutakapojitokeza chaguzi zingine.
Alisema haiwezekani waoa kama vijana ambao ndiyo jeshi la CCM na wananchi wake wakakalia kimya mambo hayo na kuhatarisha usalama wa chama,wanachama na wananchi wao katika kipindi cha chaguzi mbalimbali.
Nae mwenyekiti wa umoja huo mkoani hapo Robson Meitinyiku alimuahidi Nangole kutorejea kwa vitendo hivyo chini ya uongozi wake kwakua nao ni vijana na mbinu chafu pia wanazijua pamoja na kupambana na wafuasi hao.
Alisema mbali na kujibu mapigo hayo pia watatumia nafasi yao kama jeshi la chama katika kuhamasisha vijana wake,wanawake na wazee kujitokeza mapema kupiga kura pamoja na kuwalinda ili kuwzesha chama kuendelea kushika dola.
“mwenyekiti nikuhakikishie kwamba suala hilo halitajirudia tena tumejipanga vyema vijana watawahi kupiga kura ili wawalinde mama zetu na wazee wetu hayo yaliyojitokeza yatakua historia tuu”alisema Meitinyiku.
Aidha alimuahidi mwenyekiti huyo kuwa chama cha  mapinduzi kitalirejesha jimbo la Arusha iwapo uchaguzi utarudiwa kwakua kwasasa jumuiya yake imejipanga vyema baada ya kutambua madhara ya jimbo hilo kwenda upinzani ikiwemo hata wao kama vijana kuporomoka kiuchumi.
Katika kikao hicho wajumbe wa watano walichaguliwa kuunda kamati ya utekelezaji ambapo kwa wilaya ya Arusha alichaguliwa Amina Msangi,KaratuJackob Doday,wilaya ya Meru Titto Nassari,Arumeru Noel Severe na Monduli Diwani Kimey huku katika nafasi ya katibu hamasa alichaguliwa kwa mara nyingine mtoto wa mbunge wa Monduli Edward Lowassa,Fred Lowassa

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates