JAMII imetakiwa kujiunga kwenye vikundi vya
benki ya jamii vijijini (Vicoba) na vikundi vya kuweka na kukopa (Saccos) ili
wajiwezeshe kiuchumi kwa kupitia mikopo mbalimbali inayotolewa kupitia taasisi
hizo za fedha.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa mtaa wa
Songambele sokoni,Mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Abdon
Casmiry (Chavda) wakati akisimamia uchaguzi wa kikundi cha Mshikamano Vicoba.
Casmiry alisema kuwa ili jamii iweze kunufaika
kupitia mikopo mbalimbali inatakiwa wajiunge katika vikundi,kuliko kuwa mmoja
mmoja kwani Serikali haina uwezo wa kuwasaidia zaidi ya kujiunga kwenye vikudi.
“Serikali haiwezi kuwakwamua kiuchumi wananchi
wake kwa kupitia mikopo bila kujiunga kwenye taasisi mbalimbali za fedha,ikiwemo
vicoba na saccos hivyo jamii inatakiwa wajiunge ili waweze kunufaika,” alisema
Casmiry.
Awali,akitangaza matokeo ya uchaguzi
huo,alisema Rose Makundi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kikundi hicho cha
Mshikamano vicoba,kwa kupata kura 11 baada ya kumshinda Eveta Given aliyepata
kura 10.
Alisema Laurent Lowrri alichaguliwa kuwa
Katibu kwa kupata kura 21 dhidi ya Said Mlangi aliyekosa kura kwa kupata 0 na
Veneranda Abdon ambaye hakuwa na mpinzani alichaguliwa kuwa Mweka hazina kwa
kupata kura zote 21 .
Alisema Rashid Hamis alichaguliwa kuwa mtunza
nidhamu wa kikundi hicho kwa kupata kura 19 dhidi ya Philipo Materu,aliyepata
kura mbili na mjumbe wa kuwawakilisha kwenye benki ni Jane Casmiry.
Alisema kuwa,wahesabuji fedha ni Glady Daud na
Philipo Materu na washika funguo ni Isihaka Omary,Mariam Athuman na Evetha
Given na mjumbe wa kuwakilisha kikundi hicho kwenye shirikisho alichaguliwa
Said Mlangi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia