KAMPUNI ya Bia Tanzania Breweries Limited (TBL), imeshinda
kesi inayohusisha malipo ya Sh25 bilioni dhidi ya Kampuni ya
Serengeti Breweries Limited (SBL) katika hukumu iliyotolewa na Baraza la
Ushindani nchini (FCT).
Tume ya Ushindani nchini, mwaka 2010 iliitoza
faini ya asilimia tano ya mauzo TBL, kwa kujihusisha na tabia kinzani
za ushindani wa biashara dhidi ya (SBL), asilimia hiyo inafikia takriban
Sh25 bilioni.
Kutokana na uamuzi huo, TBL kupitia mawakili wake ambao ni Dk Ringo Tenga na Fayaz Bhojan walikata rufani.
Katika rufani hiyo, mawakili hao wa TBL
waliwasilisha hoja mbalimbali, ikiwamo ya FCC haikuundwa ipasavyo kwa
mujibu wa sheria na kwamba mwenyekiti wake, Nikubuka Shimwela
hakuteuliwa kama inavyostahili.
Mawakili hao waliendelea kudai kuwa, Mwenyekiti
huyo aliteuliwa na Waziri wa Biashara siyo Rais wa nchi kama sheria ya
ushindani inavyoelekeza, hivyo kufanya uamuzi uliotolewa kuwa batili
na unastahili kufutwa.
Licha ya hoja hizo, mawakili hao wa TBL pia walidai kuwa, Mkurugenzi huyo wa FCC naye hakuteuliwa kihalali.
Jopo la watu watatu, lililoongozwa na Jaji wa
Mahakama Kuu, Razia Sheikh lilisikiliza rufani na kukubaliana kuwa FCC
kwa kipindi hicho haikuwa imeundwa kwa mujibu wa sheria, hivyo uamuzi
wa TBL kutoa faini hiyo haukuwa halali.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia