Meneja Masoko wa kampuni ya Megatrade Ivestment Goodluck Kway akikabidhi
vifaa vya shule pamoja na vifaa mbalimbali kwa watoto wanaoishi katika
mazingira magumu katika kituo cha pasadiso mpya jijini Arusha 21
disemba 2012
KAMPUNI ya Megatrde Ivestment
kupitia kinywaji chake cha K-vant Gin imetoa misaada ya vitu mbalimbali
ikiwemo chakula kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwaajili
ya sikukuu ya krismasi na mwaka mpya katika kituo cha Paradiso mpya
jijini Arusha
Akikabidhi msaada huo jana
kituoni hapo Meneja masoko wa kampuni ya Megatrade Ivestment Goodluck
Kway alisema kuwa kampuni imejiwekea utaratibu wa kurudisha faida kidogo
wanayoipata kwa jamii hasa katika makundi maalumu kama watoto
wanaoishi katika mazingira magumu katika vituo vya kelelea sanjari na
watu wenye uhitaji
Alisema msaada huo umeweza
kugharimu shilingili Milioni moja ambapo watoto hao wataweza
kusherehekea sikukuu kama watoto wengine huku akitoa rai kwa makampuni
kujitokeza kuwasadia wototo wenye uhitaji
Vifaa mbalimbali vilivyotolewa
kituoni hapo ni pamoja na mafuta ya kupikia,sukari,unga wa ngano, unga
wa ugali,mchele,maharagwe,majani ya chai,pipi,viungo,juice madaftari na
kalamu
Katika ujenzi wa jengo hilo
jipya la kituo hicho kampuni hiyo iliweza kujitolea kwa kujenga msingi
ambapo Mkurugenzi wa kituo hicho Christopher Kaaya alimpa shukrani
Meneja masoko wa kampuni hiyo kwa kuweza kuwakumbuka mara kwa mara
Kaaya alisema kuwa kituo hicho
kinawatoto 20 ambapo hadi sasa wanasoma katika shule mbalimbali za
Internation Mkoani hapa huku akitoa rai kwa watu pamoja na makampni
kujitolea kusaidia kituo hicho chenye uhitaji wa karo za shule,vifaa vya
shule,
“Tunahitaji msaada wa kuwekewa milango ya vyoo 12 havina milango pamoja na kuzungushiwa mikanda ilikukamilisha ujenzi wa jingo
Meneja Masoko wa kampuni ya Megatrade
Investment Goodluck Kway akimkabidhi misaada mbalimbali ikiwemo vifaa
vya shule iliyotolewa na kampuni hiyo kwa Mkurugenzi wa kituo hicho
Christopher Kaaya
Wafanyakazi wa kampuni ya Megatrade wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa kituo hicho
Mkurugenzi wa kituo hicho Christopher
Kaaya akimshukuru Meneja Masoko Goodluck Kway kwa kuweza kuwaletea
misaada mbalimbali kituoni hapo
Hapa Meneja Masoko wa kampuni hiyo akiwa anamkabidhi Mkurugenzi wa kituo hela kwaajili ya nyama
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia