HAYA NDO BAADHI YA MWENENDO WA KESI YA LEMA
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (wapili kulia)
akiambatana na wafuasi wa Chadema wakitoka nje ya Mahakama ya Rufaa
jijini Dar es Salaam jana, baada ya kusikilizwa rufaa yake ya kupinga
kuvuliwa ubunge wake. Picha na Michael Jamson
Lema alivuliwa ubunge April 5, 2012, katika hukumu iliyotolewa na Jaji
Gabriel Rwakibalia, kufuatia kesi iliuyofunguliwa makada watatu wa Chama
cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel,
wakipinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
WAKILI wa Serikali Mkuu Timon amedai kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilikosea kutengua ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, kwa madai ya kutumia lugha za matusi kwa kuwa Bunge limeruhusu wanasiasa kutukanana kwenye kampeni.
Wakili Vitalis alitoa madai hayo jana, wakati wa
usikilizwaji wa rufaa ya Lema, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),katika Mahakama ya Rufani
jijini Dar es Salaam.
Wakati wakili huyo wa serikali akitoa madai hayo,
Wakili wa wajibu rufaa, ambao walishinda katika kesi ya msingi, Alute
Mughway, naye alidai kuwa Mahakama Kuu, Arusha ilikosea katika uamuzi
wake, pamoja na mambo mengine, kwa kukataa baadhi ya madai yao.
Lema alivuliwa ubunge April 5, 2012, katika hukumu
iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalia, kufuatia kesi iliuyofunguliwa
makada watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Happy Kivuyo
na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2010.
Lema kupitia kwa Wakili wake Method Kimomogoro
alikata rufaa Mahakama ya Rufani, lakini Novemba 8, 2012 mahakama
ilitupilia mbali rufaa hiyo baada ya kuini kuwepo kwa dosari za
kisheria, kutokana na pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufaa.
Hata hivyo mahakama hiyo ilimpa nafasi nyingine
ya kukata rufaa tena baada ya kumpa siku 14 kufanya marekebisho ya
dosari hizo za kisheria na kuiwasilisha mahakamani ndani ya muda huo,
amri ambayo aliitekeleaza.
Wakati Lema akikata rufaa kupinga hukumu ya
Mahakama Kuu kumvua ubunge, wajibu rufaa nao walikata rufaa (Cross
Appeal) kupinga uamuzi wa mahakama hiyo, huku wakibainisha hoja nne.
Katika hoja ya kwanza hadi ya tatu walidai kuwa
Jaji alikosea katika hukumu yake kwa kuchanganya vituo vilivyotolewa
ushahidi na mashahidi wanne na hatimaye akakataa ushahidi wapo, pamoja
na tarehe za ratiba ya kampeni ya CCM nay a Chadema.
Hoja ya nne walidai kuwa Jaji alikosea kwa kuamua
kuwa hata kama Lema kwenye kampeni zake alidai kuwa Dk. Buriani ni mkazi
wa Zanzibar hatafaa, wakidai kuwa ukazi si sifa ya kuchaguliwa kuwa
mbunge.
Hatimaye rufaa hizo zilisikilizwa jana na jopo
la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, lililoundwa na Jaji Salum
Massati, Jaji Bernard Luanda, chini ya uongozi wa Jaji Nathalia Kimaro.
Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, mawakili
wawili ambao ni ndugu, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu na kaka
yake Mghway, walipambana vikali kwa hoja za kisheria.
Lisu, Kada wa Chadema ambaye pia ni Mnadhimu wa
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alikuwa akimtetea Lema mrufani (Lema),
akisaidiana na Wakili Method Kimomogolo, huku Mughway akiwatetea wajibu
rufani ambao ni makada wa CCM.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia