Ticker

6/recent/ticker-posts

WABUNGE WAOMBA SEREKALI ZA NCHI ZA EAC KUHAKIKISHA GESI NA MADINI INAWANUFAISHA WAZAWA WA NCHI HIZO


WABUNGE wa Bunge  la Afrika Mashariki (EALA)  wameziomba nchi za EAC kuhakikisha madini ya,gesi na mafuta zinawanufaisha wananchi badala ya madini hayo kugeuka kuwa vita na uhoro wa madaraka miongoni mwa viongozi mbalimbali wa nchi hizo .
 
Pia wamehoji kama nchi za Afrika zinautajiri mkubwa wa maliasili na Utalii ni kwanini wananchi wanakuwa maskini na wazungu ambao wanachuma mali zetu wanakuwa matajiri huku waafrika baadhi wakiuwawa kutokana na uroho wa baadhi ya viongozi wanaotaka mali badala ya utu na maendeleo ya jamii.
 
Hayo yalisemwa juzi Jijini hapa na wabunge mbalimbali wa EALA wakati walipokuwa wakichangia mjadala wa Kamati ya Kilimo ,Maliasili na Utalii uliowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Isabelle Ndahayo kutoka Nchini Burundi .
 
Ndahayo alisema Nchi za Afrika zinautajiri mkubwa wa maliasili ,madini na gesi lakini bado watu ni maskini huku baadhi ya nchi watu wakipigana kutokana na uroho wa mali na kusahau wananchi wananufaika vipi na mali zinazotokana na nchi wanazoishi na baada ya kusoma ripoti hiyo katika nchi za EAC na utajiri wa maliasili kwa kila nchi wanachama aliwasilisha hoja hiyo na wabunge nao wakachangia.
 
Mbunge Adam Kimbisa  katika ripoti iliyowasilishwa imeonyesha nchi za Afrika zinautajiri mkubwa wa madini ya gesi,vito na nk lakini chakushangaza rasilimali hizo haziwanufaishi wananchi wake badala yake imekuwa ni balaa kwa nchi za Afrika kwani badala ya viongozi kubuni maendeleo baadhi yao wanakuwa waroho wa mali na kupelekea nchi kuwa maskini.
 
Alisema ni vyema sasa nchi za Afrika zikaangalia uwezekano wa wananchi kunufaika badala ya kugeuza nchi za Afrika kuwa za mapigano kutokana na rasilimali wanazozalisha na kuwaomba wabunge wa Tanzania kuhakikisha wanasimamia mikataba yote mikubwa ambayo inakuwa na manufaa kwa watanzania badala ya kuipitisha kiholela na kuleta hasara kwa Taifa.
 
”Hivi huu utajiri wa Afrika ni bahati au ni balaa …. maana wengine wanapigana wengine wanawaza wapi leo wataendesha maisha yao kwanini tusitumie rasilimali tulizonazo kuwanufaisha watu wetu,tuache mapigano bali tuangalie nchi inanufaika vipi na rasilimali zilizopo”.
 
Naye Shy-Rose Bhanji aliipongeza  kamati hiyo kwakuzunguuka nchi za EAC kujionea utajiri wa kila nchi na kutoa rai kwa nchi wanachama kuhakikisha rasilimali zilizopo zinanufaisha wananchi wake na si viongozi au watu mbalimbali kujinufaisha wao wenyewe huku wananchi wakiahangaika.

Post a Comment

0 Comments