BABA ANAESADIKIWA KUMPA MIMBA MWANAE WAKUMZAA AFIKISHWA MAHAKAMANI JIJINI MBEYA...!!!


 Mkazi wa Mtaa wa Mbete, Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(16) jina lake limehifadhiwa. akiingia mahakamani leo mbele yake ni mke wake na mtoto wake aliyezaanae ambao sura zao tumefunika
Bwana Yussuf Hamad anaetuhumiwa kuzaa na bintie akitaka kumpokonya kamera  mwandishi wa gazeti la majira Rashid Mkwinda ili asimpige picha
Jamaa kuona amezidiwa akaamua kujifunika na shati lake huku akitoa maneno makali kuwa nyie waandishi mmekosa cha kuandika mmeona hii ndiyo habari hakuna habari nyingine? alihoji mtuhumiwa huyo
Huyoooo anatoka nje ya mahakama

Sasa anavaa kofia yake ili watu wasimtambue huku akisema nifuateni niwaonyeshe kazi
Njooni sasa huku kashika jiwe
Kuona anazidi kufuatwa akaamua kuondoka mahali hapo huku  akiwa na jiwe lake mkononi
Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa huyo---
 Mkazi wa Mtaa wa Mbete, Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(15) jina lake limehifadhiwa.

Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi, Regina Simon(35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi  wa mtaa huo Bwana Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Angelo Sanga.
Viongozi hao wa mtaa walimuita  mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio hilo,lakini mtuhumiwa alikanusha ingawa binti yake alithibitisha kutendewa ukatili huo na kwamba alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.
Baada ya uongozi kupata maelezo kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa waliamua kuipeleka kesi hiyo Polisi,ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha binti huyo kupelekwa kwa 
daktari ambaye alithibitisha kuwa binti huyo ana ujauzito.


 Binti huyo amejifungua mtoto wa kike ambae sasa anamiezi mitatu mtoto huyo kaletwa leo mahakamani kama ushahidi kesi hiyo imeairishwa mapaka tarehe 12/12 mwaka h

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia