Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimesema kinasubiri kwa hamu kuona ushahidi uliokusanywa na Chama Cha Wananchi (CUF) wenye mazingira ya uhalifu dhidi yq ubinadsmu hatimaye ukubakike kimashitaka ukiikabili Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mahakama ya Uhalifu wa Makosa ya Jinai (ICC ) huko The Hague, Uholanzi
ADC kimeeleza kuwa wanachokifanya viongozi wa CUF wakati huu ni kujaribu kuihadaa dunia , nchi wahisani na jumuiya ya Kimataifa ili ionekane Zanzibar kuna mgogoro wa kisiasa unaotokana na uchaguzi mkuu uliopita.
Mwenyekiti wa Taifa wa Adc Hamad Rashid Mohamed ameeleza hayo katika mahojiano maalum na Raia Tanzania yaliofanyika huko nyumbani kwake Mbweni nje kidogo ya mjini Unguja jana.
Hamad alisema kwa kadri ajuavyo ni kwamba dhana ya kuundwa Mahakama ya Uhalifu wa Makosa ya Jinai (ICC )huambatana na matukio yq vitendo vya uhalifu kinyume na ubinadamu jambo ambalo anaamini katika uchaguzi mkuu uliopita hakukuwa na matukio ya aina hiyo huku akisisitiza kuwa kama ni suala la kujitoa na kususia uchaguzi viongozi wa CUF wanaostahili kubebeshwa lawama zote .
Alisema kwanza haiwezekani kushitaki Zanzibar ICC kwasababu si dola na ili Tanzania iweze kusimamishwa mahakamani lazima kuwe na vielelezo halisi na si ushahidi wa kutunga, kupika au wa kubuni
"Nimesikia wenzetu CUF wameandika ripoti kuhusu ukiujaji na uvunjaji wa haki za binadamu uliofanyika zanzibar , watamshitaki Waziri wa Mambo ya Mdani na IGP, tunaisubiri ripoti hiyo kwa shauku ili tuone uhalifu ulivyotebdeka "alieleza Hamad ambaye ni miongini mwa waanzilishi wa CUF mwaka 1992.
Hamad alisema kuibuka kwa ripoti hiyo bila shama ni baada ya kususia na kushindwa uchaguzi mkuu huku akisisitiza iwapo Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) ingemtangaza mgombea urais wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad anasema ripoti hiyo pengine isiingefiriwa kuandikwa .
Akizungumzia msimamo wa chama hicho kinachowataka wafanyabishara kutolipa kodi, kutokata leseni na wakulima kutouza mazao yao Serikalini,Mwenyekiti huyo wa Adc ameufananisha mradi huo sawa na kuwakaangia mbuyu wakulima na wafahyabiashara ili wafilisike kiuchuki au wakabiliwe na kesi mahakamani.
"Ni kosa kwa kiongozi ambaye analipwa marupurupu na serikali kutokana na kodi za wananchi, awe na ujasiri wa kuwazuia wananachi wasilipe kodi,haistahili kiongozi bora kutenda hayo ,hata baada ya siasa yapo maisha mengine "alisema Hamad.
Hata hivyo akizungumzia utendaji wa kazi za serikali tokea ateuliwe na Rais Dk Ali Mohamed Shein kuwa Waziri kilimo, uvuvi ,mifugo na maliasili, Hamad anasema anafurahia kufanya kazi na Rais Dk shein na kwamba kiongozi huyo ni muumini wand hana ya utendaji wa pamoja na mpenda mashirikiano kwa maslahi ya pamoja.
"Nihusudu aina ya utendaji wa Rais ,siku zote ukimuona mtu anapenda kuheshimu kanuni na taratibu huyo ni makini na hapendi kona kona, ni kiongozi shirikishi anayependa kumsikiza kila mmoja kwa wakati husika "alieleza
Kuhusu kujitokeza sintofahamu ya watu hususan Pemba kubaguana haususan katika usafiri na utoaji wa huduma , kutouziana bidhaa huku wengine wakikosa kuzikana na kushirikiana,Hamad amevitaka vyombo vya dola kusimamia sheria za nchi bila kuyumba au kufanya upendeleo.
Alisema ikiwa mfanyabiashara hataki gari lake litoe huduma kwa wananchi aliweke nyumbani kwake,anakataa kuuza bidhaa asifungue duka au genge lakini ikiwa anatoa huduma kwa ubaguzi mtu huyo akiwa Adc,CUF, CCM ,AFP au chama chochote Aashughulikiwe kwa mujibu wa sheria za nchi .
"Ubaguzi, upendeleo, maonevu na manyanyaso hayawezi kusamehewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi , kuyaacha mambo hayo yashamiri na kustawi ni hatari ijayo katika jamii ya sasa na wakati mwingine wowote "alieleza Hamad
ambaye ni mmoja kati ya waasisi wa mageuzi ya kidemokrasia visiwani humu.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia