mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema Molel ambaye pia ni mwaandaaji wa tamasha la vijana akiwa anasalimiana na wachezaji wa moja ya timu ambazo zimeshiriki tamasha hilo
Aly Mtumwa katikati akiwa anabadilishana mawazo na Aliekuwa mgombea wenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Emanuel Makongoro
Alikuwa mgombea ubunge wa viti maalumu wazazi kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi ,ambaye pia ni mkurugenizi wa Phideintatament Phidesia Mwakitalima akiwa anasalimiana na timu kabla ya mechi za siku hiyo kuanza
muandaaji wa mashindano hayo wa kwanza kulia Neema molel akifuatana na mkufunzi ambaye ni mkurungezi wa kituo cha kukuza vipaji vya vijana (Rolling stone)Ally Mtumwa tayari kwa kukagua timu kabla ya mechi kuanza
naye muimbaji wa nyimbo za injili Neema Kasambale nae pia aliudhuria kuangalia jinsi vijana wanavyo sakata kabumbu
mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema Molel ambaye pia ni mwaandaaji wa tamasha la vijana akiwa anasalimiana na wachezaji wa moja ya timu ambazo zimeshiriki tamasha hilo
wachezaji wakiendelea kusakata kandanda ndani ya kiwanja cha ngarenaro mkoani arusha
mashabiki pia waliudhuria kuangalia baadhi ya mechi
Na Woinde Shizza,Arusha
vijana wametakiwa kujijengea tabia ya kushiriki michezo mbalimbali kila mara badala ya kujiingiza katika makundi mabaya ya wizi pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya kitu ambacho kinawaaribia mfumo mzima wa maisha yao.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema Molel ambaye pia ni mwandaaji wa Tamasha vijana la mpira wa miguuu linaloendeshwa kwa mfumo wa ligi ya mpira wa miguu linayowashirikisha vijana kutoka katika kata ya sakina .
Alisema kuwa yeye kama mama anaumia sana kuona vijana wanakaa mitaani na kujiingiza katika vitendo mbalimbali mbali ikiwemo wizi pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevywa ivyo ameamua kuanzisha ligi hii ili kuwasaidia vijana wengi kushiriki na kuachana na makundi .
"unajua pia michezo ni ajira hivyo nimeona ni vyema mimi kama mama kiongozi wa watoto nianzishe ligi hii ya mpira wa miguu ili awa vijana wetu waweze kushiriki,kujifunza na pia ule mda walikuwa wanatumia kwenda kuangaika uko mtaani na kutumia madawa ya kulevywa watakuja apa watashiriki michezo "alisema Neema
Aidha alibainisha kuwa ligi hii aitaishia kipindi hichi kwani itakuwa endelevu na ameamua kuanza na watoto wa kiume kwa kuanzisha mpira wa miguu lakini pia anania yakuanzisha ligi ya wanawake ya mpira wa pete ili pia kuwawezesha watoto wakike nao kujitokeza na kujifunza kwani michezo pia ni ajara pamoja na afya.
Kwa upande wake Aliekuwa mgombea wenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika siku hii ya uzinduzi wa mashindano hayo Emanuel Makongoro alisema kuwa amefurahishwa sana kuona jinsi vijana walivyojitokeza kushiriki ligi hiii kwani wametambua umuimu wa michezo katika afya zao.
Aliwasihi vijana kuachana nakujishulisha na biashara za madawa ya kulevya pamoja na unywaji wa pombe za makaratasi(viroba) badala yake washiriki katika michezo mbalimbali na hata kama amna ligi basi washiriki katika mazoezi kwani wakifanya mazoezi yanaweza kuwasaidia kuondokana na vishawishi mbalimbali vinavyoweza kuwapata .
Kwa upande wa aliyekuwa mgombea ubunge viti maalumu wa wazazi CCM mkoa wa Arusha Phidesia Mwakitalima alisema kuwa timu hizo bado zinakabiliwa na changamoto nyingi hivyo wanaitaji wadhamini na wafadhili wakubwa kujitokeza ili kuweza kunyanyua vipaji vya vijana hao wa Kata ya sakina pamoja na Kata zote za mkoa wa Arusha
Aidha alisema kuwa wakiwawajenga vijana katika michezo itasaidia kupunguza makundi mabaya mitaani na kupelekea vijana kujituma.
Ligi hii ya Tamasha la vijana wa Sakina limeanza rasmi mapema mwanzoni mwa mwezi huu na inatarajiwa kumalizika jumapili ambapo mshindi atapatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo makombe ,jezi pamoja na mipira .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia