NA WOINDE SHIZZA, KARATU.
WATU
WA JAMII YA WAWINDAJI WAOKOTA MATUNDA NA WALINA ASALI KUTOKA KABILA LA
WAHAZABE KATIKA KIJI CHA ENDAMAGH WILAYA YA KARATU ,WAMELALAMIKA KITENDO
CHA KUTENGWA KUINGIZWA KWENYE MPANGO WA RUZUKU KWA KAYA MASIKINI
,UNAOENDESHA NA TASAF WAKATI WAO NI JAMII MASIKINI ZAIDI, KWANI KATI
YAO NI KAYA SABA TU NDIZO ZILIZO INGIZWA KWENYE MPANGO ,HIVYO
WANALAZIMIKA KUGAWANA KIASI KIDOGO WANACHO KIPATA.
WATU
HAO WA KABILA LA WAHAZABE WAMETOA KAULI HIYO KATIKA KIJIJI CHA
ENDAMASH,WALIPOTEMBELEWA NA MAAFISA WA TASAF KUTOKA MAKAO MAKUU, PAMOJA
NA WAWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA, AMBAPO WAMEDAI SASA WANALAZIMIKA
KUGAWANA FEDHA ZINAZO TOLEWA KWA KAYA SABA KWAKUWA WOTE HAWANA UWEZO NA
MATUNDA NA WANYAMAPORI WAMEADIMIKA KUTOKANA NA UKAME .
KWA
UPANDE WAKE MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA BI BILLAR BIRD AMESEMA
AMESIKITISHWA NA HALI WALIYO NAYO WATU HAO, LAKINI AMECHUKUA MAOMBI YAO
NA ATAYAFIKISHA KWENYE KIKAO CHA NCHI WAFADHILI WANAOTARAJIA KUKUTANA
MWEZI UJAO.
MKURUGENZI
MTENDAJI WA TASAF LADISLAUS MWAMANGA AMESEMA KASORO HIZO ZIMETOKANA NA
TABIA YA JAMII HIYO YA KUHAMAHAMA NDIYO MAANA WALIKOSA FURSA HIYO
LAKINI TASAF ITAANGALIA NAMNA YA KUWASAIDIA.