MEYA NA MKURUGENZI WA TANGA WAPEWA ONYO KALI

 Mstahiki Meya Wa Jiji la Tanga Mustafa Mhina akizungumza na kumhakikishia Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa ya kua kamwe hawezi kuyumbishwa na upinzani na Anawaahidi wana Tanga kufanya kazi kikamilifu ili kuleta maendeleo katika Jiji la Tanga.




Na Woinde Shizza,Tanga

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeitaka halmashauri ya Manispaa ya Mji wa Tanga kuitisha vikao vya madiwani kama kawaida na kumtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo atimize wajibu wake ipasavyo kabla hajachukuliwa hatua za kisheria .

Imeelezwa kuwa haiwezekani kwa mtumishi yeyote  aliyeajiriwa na serikali ya ccm akawa mzandiki, adui na msaliti wa sera za serikali ya chama tawala.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameeleza hayo  wakati akizungumza na wanachama wa uvccm na ccm kwenye ukumbu wa TANU Hall mjini hapa.

Alisema ni jambo la kushanagaza kuona vikao ambavyo ndivyo vinavyotakiwa kujadili, kupanga mipango na kutekeleza program za maendeleo vikiwa haviitishwi kwa muda mrefu  kwasabahu za kipuuzi zisizo na mashiko.

"Tunasikia  Meya wa Manispaa ya Tanga kupitia ccm kwamba CUF wana mpango wa kukununua ili uhame  ccm , tunakwambia kama kuna mkakati huo kataa, CCM  ni chama kikubwa, mikono yake ni mirefu "alisems Shaka.

Shaka alimtaka Meya wa Manispaa ya Tanga Mustafa Seleboss kuhakikisha vikao hivyo vinaitishwa na chama chochote kitakachojaribu kukwamisha  uvccm watapambana nacho.

Alisema si haki wala wajibu ikiwa kikao halaki cha madiwani kimemchagua mstahiki  Meya  wa mji Tanga  kwabtaratibu halali kilifanyika na matokeo yakakipa ushindi ccm hivyo tishio lolote la vurugu au la kukwamisha maendeleo ya wananchi  halitakubalika.
"Wana ccm na uvccm acheni kulalamima kila siku kwamba kuna baadhi ya viongozi na  waliosaliti bila kuwachukulia hatua za kinidhamu na kimaadili, akipatikana msaliti kwa ushahidi kamili mtoseni ili tusonge mbele"alisema.

Aidha Shaka alisisitiza kuwa kila mtendaji au Mkurugenzi wa halmashauri ana wajibu wa kusimamia maelekezo ya kisera katika utendajikazi  wake pamoja na kufuata taratibu za kisheria husika

Kwa upande wake mstahiki Meya selebos akijibu  madai ya Sgaka alimhakikishia kuwa hakuna mpinzani au chama vjochote chenye chenye ubavu na jeuri ya kumnunua na kumtoa ccm.

Mstahiki huyo Meya alikiri kuwa ni kweli wapo baadhi ya watendaji wa ngazi za serikali wanaoonekana kuwa waasi wasiotii matakwa na utashi wa kutoitumikia serikali ya ccm kwa.

Seleboss alisema hata hivyo pamoja na vikwazo vilivyopo katika baadhi ya maeneo na kuwepo kwa watendaji  watukutu alisema anaamini serikali itachukua nafasi yake kuwakabili na kuwadhibiti.

Jumla ya wanachama wapya wa uvccm kutoka Chuo cha utumishi Kange mkoani Tanga kwa hiari yao walijiunga na umoja huo pamoja na kumtawaza rasmi kamanda mpya wa uvccm Mkoa wa Tanga Najim Senga.
Picha ya pamoja ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka Wazee Waasisi Mkoa wa Tanga





Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post