Mbunge wa Karatu Wile Qambalo.
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Karatu Jubilate Mnyenye.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Omary Kaang.
Na Woinde Shizza,Karatu
Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Karatu limewasimamisha kazi
baadhi ya watumishi kutokana na ubadhilifu wa fedha za Umma.
Mwenyekiti wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Karatu Jubilate
Mnyenye amewataja waiosimamishwa ni Dr.Thobias Nkina ambaye alikuwa
mganga mkuu,Judas Mahuma -Afisa Ardhi, George Ndimbo aliyekuwa
Mhasibu,Jonathan Rukuntuka-Mtunza fedha,Sigfred Njanga-Mtunza
fedha,Rajabu Lingoni alikuwa Muweka Hazina na Gurisha Kavuga -Mtunza
stoo, wote hawa wamesimamishwa kwaajili ya uchunguzi.
Amesema kuwa kutokana na tume ya uchunguzi iliyoundwa mwezi mmoja
uliopita na kamati ya fedha ya Halmashauri ,ikitaka kufahamu mapato na
matumizi ya Kilimo na Afya ,ilibaini mambo kadhaa ambayo iliwasilisha
kwenye.kikao kwaajili ya maamuzi,ndipo kamati ya madiwani ilipoamua
kuchukua hatua ya kuwasimamisha .
Sambamba na hayo wapo watumishi ambao wamepewa onyo ambao ni Afisa Elimu
Bernad Mnyenyelwa, Dr.Kyabaroti Kyabaroti pamoja na Omari
Shemdiru,ambapo wapo watumishi wengine 8 ambao wanapaswa kurudisha fedha
walizozichukua shilingi milioni 81 kama masurugu ya kufanyia shughuli
mbalimbali za idara zao ndani ya siku 14.
Kwa maelezo ya baraza la madiwani limeomba wizara inayohusika kwa
mkutugenzi huyo imuwajibishwe kwa kuisababishia Halmashauri hasara ya
milioni 800 na kushindwa kuwasimamia watumishi wake na huku miradi ya
kilimo na Afya ikiathirika.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Moses Mabula.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Moses Mabula amesema kuwa alipohamia
katika.Halmashauri ya Karatu mwaka 2013 alikuta zimetumi zaidi ya
milioni 200 pia ameongeza kuwa Halmashauri iliazima fedha kwaajili
yakutekeleza miradi ya dharura,kati ya miradi hiyo ni pamoja na
ukarabati wa stendi kuu ya Karatu,Zahanati ya Ayalabe iliyoungua
moto,Ujenzi wa.madarasa 4 katika.shule ya msingi Ayalabe ili kupisha
chuo ,ukamilishaji wa mitaro katika jengo la.halmashauri,ujenzi wa
mahabara Endara na Mang'ola,Ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi
Manusway,Ukamilishaji wa hostel ya wasichana katika shule ya sekondari
Kansay .
Hata hivyo Moses Mabula amesema kuwa fedha zote ziliripotiwa katika
baraza lililopita la madiwani 2015,pia amesema.ameyapokea.malalamiko
yote na atawajibu baraza namna fedha zilivyotumika.