Mbunge
Shyrose Bhanji wa Tanzania akichangia mada bungeni
wabunge mbalimbali wakichangia mada bungeni wakati bunge la bajeti ya jumuiya ya afrika mashariki likiendelea
wabunge wakijadiliana jambo wakati bunge likiendelea
.
Na Woinde Shizza,Arusha
Wabunge wa bunge la Afrika mashariki wamesema kuwa wanamuunga mkono rais wa jamuhuri ya Mungano wa Tanzania John Magufuli na watampa ushirikiano katika kila jambo kwani anafanyakazi kwa makini na vizuri .
Pamoja na kumpongeza na kumuunga mkono Magufuli pia wameomba kukutana nae na kujadili baadhi ya mambo .
Wakiongea na waandishi wa habari wabunge baadhi ya wabunge hao walisema kuwa wanafurahishwa sana na kasi ya magufuli kwani imekuwa na manufaa makubwa sio kwa watanzania pamoja na wananchi wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki kwa ujumla
" kasi ya Rais Magufuli, imekuwa na
manufaa makubwa sio kwa watanzania bali kwa wananchi wote wa jumuiya ya
Afrika ya Mashariki"alisema Mbunge
Shyrose Bhanji wa Tanzania,
Aliongeza kuwa vita
dhidi ya rushwa na ufisadi ambayo imeanzishwa na Rais Magufuli, ambaye
pia ni mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, inapaswa kuungwa mkono na bunge
hilo.
Mbunge
Martin Ngoga wa Rwanda, alisema kasi ya Rais Magufuli ambaye ni
mwenyekitiwa jumuiya hiyo,inapaswa kuungwa mkono na sio vibaya jumuiya
ya Afrika ya Mashariki, kuonesha kwa dhati inapambana na rushwa.
"Rais
Magufuli anafanyakazi nzuri sana na sisi kama wabunge tunamuuunga mkono
ili kuwa na manufaa katika jumuiya ya Afrika ya Mashariki mataifa yote
yanapaswa kushirikiana kuondoa rushwa"alisema