VIJANA WATAKIWA KUIGA MAMBO MEMA

 Kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anaongea na wananchi wa mkoa wa Tanga katika mkutano wa adhara
 Shaka akiwa na vingozi wengine waki sikiliza kero za wananchi


Na Woinde Shizza, Tanga

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Kassim Mbuguni amesema ujasiri ,
uhodari na ukomavu wa maarifa alionayo Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM
Shaka Hamdu Shaka unahitaji kuigwa na vijana wenzake wakati huu ambapo
serikali  na chama vikiwa katika mchakato wa kujipaanga kuleta
mabadiliko ya msingi.

Amesema kila anapotokea kijana ndani ya CCM  ambaye ana nguvu za
utetezi kwa yale anayoyaeleza, anayoeneza na kuyawekea msimamo kwa
niaba ya jumuiya yake na chama huo ni ushupavu mpya.

Mbuguni alieleza hayo wakati akitoa neno la shukran mara baada ya
shaka kuhutubia wanachama wa UVCCM na jumuiya zake katika ukumbi wa
TANU Hall mjini hapa.

Alisemakuwa  amefarijika sana kumsikia kijana mdogo na mchanga katika
siasa za nchi akizungumza kwa kujiamini, kuelekeza kutokana na
miongozo, taratibu na kikanuni  huku akitoa misimamo inayokwenda ma
mahitaji ya wakati uliopo .

"Nimepata matumaini mengine kwamba hazina yetu  ya kisiass na makada
wake haifikisiki wala kufiiisika "alisema Mbuguni.

Aidha aliwataka vijana wa wikaya Tanga na maeneo  meingine ya nchi
kufuata nyayo za kiongozi wao ambaye ameonyesha ana dhamira, malengo
na amejitoa kwa ajili ya kuitumikia nchi.

Mwenyekiti huyo wa CCM wilaya Tanga amesisitiza  kuwa aina ya uongozi
wa vijana kimsingi  ina tofauti na ule wa wazee kwasabahu vijana ndiyo
wenye damu ya kuweza na kumudu kutenda na kuthubutu lolote kwa wakati
wowote wautakao.

Hata hivyo alisema kila wanapochomoza vijana madhuhuti aina ya shaka
aidha awe wa kike au wa kiume , CCM huongeza mtaji wake katika
uwekezaji wa kisiasa kwasababu ana uthubutu hata wa kuihoji  mamlaka
za serikali zitimize wajibu wa kutumikia wananchi bila kukawia.

"Tunapokuwa katika mtukutu wa kusaka ridhaa ya kidemokrasia toka kwa
wananchi viongozi wa CCM huwaomba watu wakipige kura chama na wagombea
wake,ole wao  wanaojigamba baada ya ushindi kwamba hawakisikilizi
chama,tutawaumbua na kuwatumbua"alisema mwenyekiti huyo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post