Waandishi wa habari wakichukua taaarifa |
Mtandao wa Tigo 4G LTE ni mpana na wa kasi
Tanzania
Dar es Salaam, Mei 4, 2016-Kampuni ya simu ya Tigo ambayo
inaendesha maisha ya kidijitali Tanzania imetangaza kuzinduliwa kwa huduma ya 4G LTE katika miji mingine mitano ya
kanda ya ambayo ni Tabora, Musoma, Bukoba, Kigoma na Shinyanga.
Kampuni hiyo
awali ilizindua huduma hiyo jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa mwaka jana na baadaye kuisambaza katika miji ya Arusha, Tanga, Dodoma, Morogoro,
Moshi na Mwanza na hivyo kuifanya kuwa
kampuni ya simu yenye mtandao mpana na
wa kasi wa 4G LTE nchini Tanzania.
Ikiwa inachukuliwa kuwa ni teknolojia
nzuri na ya uhakika katika sekta ya mawasiliano ya
simu duniani ya kupata intaneti, kasi ya
teknolojia ya 4G LTE ni takribani mara
tano zaidi ya teknolojia ya 3G na Tigo inaifanyia kazi kwa kina ili kuongeza
ubora wa huduma hiyo na mtandao wa 4G kutokana na matumizi ya wateja kuwa nayo yanaongezeka kwa kasi kubwa.
Hivi sasa Tigo ina timu inayofanya kazi saa zote kuimarisha na
kukuza ubora wa teknolojia ya 4G. Matokeo yake ni kwamba mtandao wa 4G umekuwa unategemewa kwenye miji ambamo upo (Arusha, Tanga, Dodoma,
Morogoro, Moshi na Mwanza).
Mtandao
wa 4G LTE unatoa intaneti ya kasi ya kurambaza (surf) na kupakua vitu,
kufanya miito ya simu ya kuonana (Skype) isiyo na kikomo. Kutokana na uzinduzi wa hivi karibuni wa video za bure kupitia YouTube nyakati za usiku, mtandao wa 4G LTE unawawezesha wateja kwa
kiwango kikubwa kupata uzoefu wa
kutiririsha video zilizo na uangavu mkubwa. Aidha kutokana na ushirikiano na Facebook mteja wetu wa 4G pia anaweza
kufurahia kutiririsha video zilizomo kwenye
mitandao maarufu ya kijamii
duniani.
Pia, mteja akiwa na 4G LTE
anaweza kupakua mafaili
makubwa (sinema, mafaili
yanayohusiana na kazi) au vifaa na hali
kadhalika kucheza michezo kwa njia ya mtandao.
Akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa Tigo Diego
Gutierrez, alisema mpango wa kupanua teknolojia ya 4G hadi kwenye maeneo yote ya
nchi upo mbioni ambapo kampuni hiyo
imejikita kwenye kuwapa wateja wake huduma
zenye ubora duniani ambazo
zitawawezesha kufurahia mtindo wa maisha ya kidijitali.
“Kupanua mtandao wa 4G LTE nchi nnzima kwa mara nyingine kunaonesha sio tu Tigo
kuongoza kwenye kutoa teknolojia
na ubunifu wa kisasa ndani ya
soko bali pia kusisitizia kujituma kwetu katika kuongeza fursa ya kufikia intaneti kwa Watanzania walio wengi kwa kadri iwezekanavyo,’ alisema
Gutierrez.
Kwa mwaka huu 2016,
Tigo itawekeza zaidi ya dola
milioni 75 kwenye upanuzi wa mtandao na kuimarisha ubora wake kwa kukuza maeneo ya teknolojia ya 4G na 3G,
mkongo wa mawasiliano na hali kadhalika kuongeza idadi ya sehemu za
kutolea huduma kwa wateja nchi nzima.
“Tukiwa kama
kampuni tunatambua umuhimu wa wa ubora na ukaribu kwa wateja wetu na tunafanya kazi ili kufikia malengo hayo katika siku za
karibuni,” alisema Gutierrez.
“Hivi sasa pia
tuna programu ya kufanya mtandao kuwa wa
kisasa ambao unajumuisha kuongeza uwezo wa 4G
kwenye miji yote 12 ambako tuna mtandao wa 4G pamoja na kuongeza mtandao wa 3G kufika maeneo yote nchini,”
alisema Gutierrez na kuongeza kuwa
wateja wa Tigo katika miji ya Mbeya,
Mtwara na Lindi wajitayarishe kufurahia
huduma ya Tigo 4G LTE itakayoanza
kutolewa siku za hivi karibuni.
MWISHO
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia