Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo |
Na Woinde Shizza,Arusha
Jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa tatu
wa chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la Harold Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za
uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Davis
Mwamunyange pamoja na kusambaza ujumbe
wa maneno makali juu ya viongozi hao.
Akiongelea tukio
kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo
alisema kuwa tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu majira ya saa
09:00 asubui .
Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi
kuhusu mkuu wa majeshi ambapo alimtaka
mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote
wawe nje ya nchi huku akuna kiongozi
aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.
“mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya ,Mwamunyange pindua
nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile
kiti,hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “alisema Mkumbo.
Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo piamtumiwa
huyo alisambaza ujumbe mwingine wenye maneno yafuatayo,”Dr Shein
akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji ya kisiasa
yaliyotokea Zanzibar yawe kwaviongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi
wa kawaida”hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijamii kama faccebook.
Mkumbo alisema kuwa
mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika,huku
akitoa rai kwa watu wote wanaotumia
mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo
ya kijamii pasipo kukiuka sheria
na taratiu za kisheria .
Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye
bainika anatumia mitandao vibaya na
kusema kuwa atachukuliwa hatuakali za
kisheria dhidi yake.