Na Woinde Shizza, Arusha
Viongozi wa kimila
jamii ya kimasai maarufu kwa jina la Laigwanani wametakiwa
kuacha kujiingiza katika maswala ya kisiasa kwa kutumiwa na wanasiasa ili
kudumisha mila na desturi za kabila ilo .
Aidha viongozi
hao wameaswa kuhamasisha jamii ya kabila hilo kuwapeleka watoto wao shule ili
kupata elimu itakayo wasaidia kukabiliana na changamoto za kimaisha ikiwemo swala
la ajira ambalo ni tatizo kubwa kwa jamii hiyo ya kifugaji .
Kauli hiyo
imetolewa leo Jijini Arusha na mwenyekiti wa Laigwanani .Isac l LeKisongo
katika kikao maluum cha kutambulisha uwongozi mpya uliochaguliwa hivi karibuni
wilayani Monduli kilicho jumuhisha Laigwanani kutoka wilaya 6 za mkoa wa Arusha.
Elkisongo
alisema kuwa wanasiasa wamekuwa changamoto kubwa katika jamii ya kimasai
kufuatia baadhi ya malegwanani wakijikuta wakishawishika na wanasiasa na kuweka
pembeni mila na desturi za kabila hilo zinazo wataka wasijingize kwenye maswala
hayo kwakuwa walichaguliwa kwa hajili ya kuwatumikia wananchi wote .
Mwenyekiti huyo
ambaye amechaguliwa kuwaongoza vingozi wa kimilaamesema atakikisha anasimamia
misingi ya kabila hilo kwa kurejesha eshma ya kabila hilo ambayo imeanza
kutishia kupotea na kuihasa jamii ya kabila hilo kudumisha mila yao na
kuzingatia kuwapeleka shule watoto wao.
Naye mwenyekiti
wa malegwanani tawi la Monduli Mepukori Mberekeri, alilaani hatuwa ya vijana wa
kimasai kukimbilia mjini na kujiusisha na maswala ya kusuka nywele ulinzi,na
kukata kucha wakina mama na kudai kuwa kitendo hicho kinazalilisha kabila hilo
na kueleza kuwa yeye pamoja na viongozi wenzake watangalia uwezekano wa
kuchukuwa hatuwa .
Akizungumzia
swala la viongozi wa mila kujingiza katika siasa amesema tayari wameshaanza
kuchukuwa hatua ya kuwatoza faini ya
dume moja la Ng’ombe wale wote walotekwa kisiasa na kusababisha mgawanyiko kwa
jamii hiyo.
Aidha alisema
swala la viongozi katika jamii hiyo kwa sasa ni gumu na awafikirii kumpa rungu
mwanamke kama eshma ya jamii hiyo kuongoza wanaume isipokuwa wameruhusu
wakina mama wa jamii hiyo kujingiza katika maswala ya kisiasa kushika nyazifa mbali
mbali wazitakazo.
Viongozi hao
waliochaguliwa wanatarajiwa kusimikwa na kupewa eshma juni 3 mwaka huu katika
sherehee zitakazo fanyika katika ofisi zao zilizopo eneo la chuo cha ufundi
Arusha