SHAKA :VIONGOZI WA UPINZANI BADO NI VIBARAKA VYA WAKOLONI NA MABEBERU




Na Woinde Shizza, Lushoto
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM) umesema viongozi wa
vyama vya upinzani nchini havihitaji mabadiliko na  kimaendeleo
kwasababu ndani ya vyama hivyo kumejaa  vibaraka na mawakala
wanowatumiwa na wakoloni na  mabeberu wakipinga yasitokee mageuzi kiuchumi na kiutawala.

Aidha umoja huo umewataja  baadhi ya viongozi wa vyama hivyo ni
mbumbumbu wa mambo wenye  uelewa mdogo aidha katika masa ya kihistoria
au utawala huku baadhi yao wakiwa mawakala  wa wakoloni waliopinduliwa
wasiotaka waafrika wajikomboe na kujitawala.

Hayo yamebainishwa  jana  na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu
Shaka wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika  katiKa kijiji
cha Handei kata ya Ubiri  wilayani Lushoto  Mkoani hapa katika siku ya
pili ya ziara yake mkoani humu.

Shaka alisema viongozi hao kwa muda mrefu wamekuwa wakijifanya
watetezi wa haki za wananchi na kujifanya wanapinga vitendo vya
ufisadi huku  baadhi ya mambo  wakidai yanakwenda  ndivyo sivyo.

Alisema unafiki wa wanasiasa wa kambi ya upinzani umedhihirika  baada
ya Rais  Dk John  Magufuli kuanza  kuchukua hatua makini na stahili
kukomesha vitendo hivyo lakini cha kushgaza  watu wale wale sasa ndiyo
wanaompinga na kutaka kummkwamisha wakidai anaendesha mambo kinyume na
sheria .

"Ni ajabu sana unapomsikia hata Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye
na mbunge wa Singida Mashariki  Tundu Lissu wakionyesha unafiki na
uzandiki pia kupotosha ukweli kwa lengo la kupata  umaarufu wa kisiasa
, wanajivunjia heshima na kuiporomoshea  hadhi upinzani  uonekane
hauna maana yoyote" alisema

Aidha alisema watu wenye busara waliitaraji kuwaona viongozi wa
upinzani wakimuunga mkono kwa vitendo  Dk Magufuli katika dhamira yake
ya kuleta mageuzi  kiuchumi, kiutawala na kiutendaji  kinyume chake
kambi hiyo imeamua kumtumikia shetani kwa kushiriki  usaliti na
uzandiki.

Shaka alisema kitendo cha Sumaye kudai  ati Dk Magufuli anaongoza nchi
kwa woga kwasabahu tu serikali imezuia matangazo ya bunge yasirushwe
moja kwa moja kwenye runinga  yanasikitisha na hayakustahili  yatamkee
kwenye kunywa cha mtu aliyewahi kushika wadhifa wa u- PM .

Kaimu huyo katibu mkuu alisema wakati Serikali ya Rais Dk Magufuli
akijitahidi kupambana na ubadhirifu wa mali za umma, kukomesha ufisadi
na kutaka Taifa sasa  lijitegemee kiuchumi,  Lisu anaaibisha pale
anapoukumbuka utawala wa sultan  Jamsheed wa Zanzibar aliyepinduliwa
na  waafrika ili wawe huru.

Pia Shaka alisifu Meya wa Manispaa ya Kinondoni kupitia Vhadema kwa
ujasiri , uthubutu na utayari wake wa kuungana na kasi ya Rais
Magufuli kutokana na kuwasimamisha kazi Mhandisi na Mwanasheria wa
manispaa hiyo huku uchunguzi zaidi ukiendelea .

"Lisu hana analolijua, ni Mwanasheria aliyesomea sheria ila hakupata
upeo wala maarifa yakutosha, anapokumbuka kitendo cha mkoloni  mmoja
kutaka aondoke ili mkoloni  mwingine aendelee  kuwakandamiza waafrika
wa zanzibar, Lisu anaidhihirisha dunia ni kibaraka mpya anayetumiwa na
wakoloni kwa kujijua au kutojielewa  "alisema kwa msisitizo.

Shaka alisema hatibza uhuru uliotolewa na waingereza Disemba 10 mwaka
1963 alikabidhiwa suktan Jamsheed Bin Abdullah na wala hakupewa
aliyekuwa Waziri mkuu Mohamed Shamte Hamad huku katiba ya zanzibar
ikimtaja mfalme ndiye atakayekuwa mkuu wa nchi.

Hata hivyo Shaka alimponda Lisu kwa kukubali kulishwa maneno ya
wanasiasa wa Hizbu wapya wa zanzibar ambao wanaendelea kupigania
maslahi ya vyama vya ZNP na ZPPP vyama
ambavyo vilikuwa vikitumiwa na wakoloni kwa lengo la kuendelea
kuikalia zanzibar kinyume na matakwa ya waafrika walio wengi .

Jumla ya wanachama wapya 56 wa uvccm walijiunga na umoja wa vijana  wa
cvm katika mji wa Lushoto, UWT 55 na ccm ikivuna wanachama 103 na
kupewa kadi mpya.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post