Waziri mkuu wa Juamuhuri ya muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa akiwa anasalimiana na baadhi ya viongozi mara baada ya kuwasili katika kiwanja cha ndege cha kia tayari kwa ajili ya kufungua mkutano huo |
Na Woinde Shizza,Arusha
Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu
Majaliwa kesho anatarajiwa kufungua
mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa Afrika kama nyenzo ya maendeleo
endelevu utakao fanyika katika ukumbi wa
mikutano wa kimataifa AICC jijini Arusha unaotarajiwa kufanyika kwa siku nne .
Akiongea na waandishi wa habari katibu mkuu wa wizara ya
maliasili na utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi wakati akiongea na
waandishi wa habari jijini hapa juu ya maandalizi ya mkutano huo ambao umeandaliwa
kwa ushirikiano wa serekali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na
shirika la UNESCO nakituo chake cha
urithi wa dunia.
Alisema kuwa madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto
na mambo ambayo yanatishia na kuadhiri
uhifadhi bora wa maeneo ya urithi wa dunia katika afrika .
Aidha mkutano huo utapendekeza suluisho kwa kupitia upya
shughuli zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango wa
miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi ijayo.
Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa
kushawishi wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi inayoendana na uhifadhi
wa urithi na maendeleo endelevu pamoja kuchunguza jinsi mitafaruku inayotokea
kwenye maeneo urithi wa dunia kutokana
na makundi ya kigaidi na kutunza amani utamaduni na uridhi asilia.
Aliongeza kuwa pia mkutano huo umejikita kwenye sera ya
UNESCO ya mwaka 2015 inayohusu
kujumuisha maendeleo endelevu kwenye mkataba wa uridhi wa dunia.
“mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa kisayansi, pia
uatakuwa na manufaa kwa taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kutalii na kisasa
bali pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi ya wageniwatakao
uthudhuria mkutano huu pamoja na
kuanzisha mitandao wa kitaaluma na kujenga mataji wa kijamii”alisema Malinzi
Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote kutakuwa
na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa yakifanyika siku zote za
mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa katika hifadhi ya taifa ya
Ngorongoro