BREAKING NEWS

Tuesday, May 24, 2016

JUMLA YA WATUMISHI HEWA 132 WILAYANI ARUMERU WASHIKILIWA


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Felix Ntibenda (picha ya maktaba)

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Wilson Nkhambaku, ametangaza kubaini na kuwashikilia watumishi hewa 132 ambao wamepatikana kutoka Halmashauri za Arusha na Meru zilizopo kwenye Wilaya hiyo.

Aidha, Nkhambaku amesema bado wanaendelea kuwahoji huku uchunguzi zaidi ukiendelea, na kwambw tayari akaunti zao zimefungwa lengo likiwa ni  kudhibiti kutoingiziwa tena  fedha.

Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la  Madiwani Halmashauri ya Arusha, Nkhambaku alisema kati ya hao, 28 wanatoka katika Halmashauri ya Arusha na waliobaki wanatoka Halmashauri ya Meru.

Alisema kufuatia hatua hiyo, tayari Wilaya imesharudisha zaidi ya Sh milioni 70, baada ya watuhumiwa wote  kujisalimisha na kurejesha fedha hizo, na kwamba zaidi ya milioni 10 zimepatikana Halmashauri ya Arusha na nyingine Halmashauri ya Meru.

Nkhambuka aliongeza kuwa mara  baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa wote  watakaobainika watafikidhwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili, ikiwa ni pamoja na uhujumu uchumi wa nchi.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates