baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la kumsaka mlibwende wa mkoa wa Arusha wakiwa katika pozi
warembo hao wakiwa wanacheza hii ikiwa ni moja ya mazoezi yao wanayoyafanya ndani ya ukumbi wa hoteli Naura Spring Arusha ambapo wameweka kambi
Na Woinde Shizza,Arusha
Kusimamishwa kwa shindano
la umrembo Tanzania (miss Tanzania ) kwa mwaka mmoja imekuwa ni
changamoto kubwa kwa waandaaji wa shindano hilo kwani warembo wengi
wamesahau na shindano kwa ujumla limepungaza motisha.
Hayo yamebainishwa na muaandaaji wa shindano la kumsaka mrembo wa mkoa wa Arusha kutoka katika kampuni ya
Tour Visual Entertainment Penda Simwita wakati akiongea na mwaandishi wa habari jana katika kambi ya kumuandaa Miss Arusha.
Alisema
kuwa kwa upande wake kumekuwa shindano hili limekuwa gumu kidogo kwani
warembo wengi wamejipweteka na walijisahau kuwa kunashindano kama hili
kwa mwaka huu hivyo ilimlazimu kutembelea katika vyuo mbalimbali vya
hapa mkoani Arusha kwa ajili ya kuwatafuta warembo ambao watashiriki
shindano hili.
"pamoja na kuwa tumewatafuta likini
kiukweli tumewapata warembo wazuri wanasifa na naamini wataweza kutetea
taji la miss Tanzania likatoka hapa kwani wanauwezo na kizuri zaidi
najiamini naweza kuwaandaa maana ata mrembo ambaye anashikilia taji sasa
ivi alitoka mkoa wa Arusha ,na kipindi kile kulikuwa bado kuna mrembo
wa vitongoji kwaiyo alitoka kwangu ambapo niliandaa miss Arusha City
Cetre kwa iyo naamini na uyu atatoka pia kwangu maana najua kuwapika na
kuchagua warembo wazuri wenye sifa heshima na uwezo pia wanao"alisema
Pendo.
Gazeti hili lilizungumza na
mmoja wa warembo hao Maurine Ayubu naye alisema kuwa amefurahi kushiriki
shindano hili naanao uwakika kwa kuwa anasifa zote za kuwa mrembo wa
Mkoa wa Arusha,mrembo wa kanda ya kaskazini na pia anaamini atatetea
taji la miss tanzania libaki Arusha kama linavyoshikiliwa sasa ivi na
mrembo wa Tanzania Lilian kamazima
"nasema hivyo
kwakuwa najua urembo najiamini na ninauwezo kwaiyo naamini
nitachukuwa,pia kuna ili swala watu wengi wamekuwa wakilichukulia na
kusema kuwa kuwa miss ni umalaya nataka niwatoe shaka na niwaambie
watu hususa ni wazazi umiss ni urembo kama urembo mungine na sio
umalaya kwani kila mtu anakuwa na tabia yake ambayo ametoka nayo kwao
kwa iyo akifanya kitu anafanya kama yeye na sio kwamba mrembo akiwa
malaya basi shindano hilo ndio linawafundisha la hasha bali ni tabia ya
mtu binafsi hivyo ata wazazi wasiwazuie watoto wao kushiriki shindano
hili kwa kuwa na dhana ya kuwa shindano hili ni lakimalaya"alisema
Maurine.
Jumla ya warembo 17 kutoka
katika mitaa mbalimbali na wilaya mkoani hapa wanatarajiwa kupanda
jukwaani mapema May 28 mwaka huu katika ukumbi wa Hotel ya Naura Spirng
kwa ajili ya kumsaka mlibwende wa mkoa wa Arusha ambaye atawakilisha
mkoa katika kinyanganyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania na tukumbuke
mpaka hivi sasa taji hilo la mrembo wa Tanzania linashikiliwa na mrembo
kutoka mkoa wa Arusha Lilian Kamazima .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia