NA WOINDE SHIZZA, ARUSHA.
TAASISI
YA UKAGUZI NA UTHIBITI WA VIWATILIFU TPRI IMETOA ONYO KWA WANANCHI,
KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA VYANDARUA VILIVYO INGIA NCHINI KUTOKA NJE YA
NCHI, HUKU VIKIWA NA ALAMA YA UWEPO WA DAWA YA KUUA MBU LAKINI HAVINA
MAELEZO YA KULINDA AFYA ZA WATUMIAJI NA HAVIMO KWENYE ORODHA YA MSAJILI
WA VIUATILIFU.
MSAJILI
WA VIUATILIFU DK ELIKANA LEKEI AMETOA KAULI HIYO ALIPOKUWA ANAZUNGUMZA
NA WAANDISHI WA HABARI KUFUATILIA SHEHENA YA VYANDARUA HIVYO KUINGIZWA
NCHINI, HUKU VIKIWA HAVINA MAELEZO YA TPRI HUKU AKIONESHA BAADHI YA
VYANDARUA HIVYO.
KWA
UPANDE WAO WAZALISHAJI WA VYANDARUA WAMESEMA HALI HIYO INATOKANA NA
VYANDARUA VYA NJE KUINGIZWA NCHINI BILA USHURU NA KWAMBA IMEATHIRI
VIWANDA VYA NDANI NA KULAZIMIKA KUPUNGUZA ZAIDI YA WAFANYAKAZI ELFU
MBILI.