Kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka kati kati alipotembelea kaburi la aliyekuwa mufti mkuu wa Tanzania hayati Sheikh Hamed Bin Juma Bin Hamed katika msafara wa makaburi ya Msabweni mkoani Tanga
Shaka akiwa na ujumbe wake waliozuru katika kaburi la mwandishi gwiji wa vitabu vya fasihi andishi na simulizi hayati Sheikh Shaaban Robert huku mjinimwema mkoani Tanga
Shaka akishuku kwenye treni alipomaliza kutembelea reli ya tanga kuzungumza na uongozi pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya TRL
shaka akipanda kwenye treni tayari kwa ajili ya kwenda kwenye ziara TRL
Ujumbe wa baraza kuu la Taifa UVCCM Samami Mohame kushoto kwake Kaimu katibu kuu wa UVCCM taifa Shaka na katibu wa ccm mkoa wa Tanga Shija othman Shija waliposafiri umbali wa kilomita tano toka kituo cha Tanga mjini hadi maeneo ya viwandani
Mkuu wa utawala Omar Ng'wanang'walu akiwa anashuka kwenye kichwa cha treni anyefuatia ni katibu wa ccm mkoa wa TangaShija Othman Shija |
Na Woinde Shizza, Lushoto
Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Lushoto , mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa zamani wa jimbo la Lushoto Balozi Abdi Mshangama amesema Umoja wa Vijana ndiyo moyo na uhai wa Chama Cha Mapinduzi kwa wakati uliopo na ule ujao katika mustakabali wake kisiasa na kiutawala
Amesema bila umoja huo kuwa imara kuna hatari ya kuwa na Taifa la vijana ambao aidha watakuwa legelege, waoga au wavivu ambao watakuwa wamekaokosa shime na dhati ya kuwa na fikra za kizalendo, uchapakazi na uaminifu katika Taifa .
Balozi Mshangama alitoa maelezo hayo kabla ya
kukaribishwa Kaimu katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakati
akizungumza na wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya uvccm wilaya ya
Lushoto wakiwemo na wajumbe wa kamati ya siasa ya ccm wilaya, viongozi
na wanachana wa CCM wilayani hapa
Alisema siku zote matarajio na matazamio ya chama chetu ni kuona Umoja wa Vijana ukiimarika, vijana wake wakionekana kujiituma na kufanyakazi kwa bidii ili kukipa nguvu chama na sura yenye haiba njema kwa uimara wa chama na serikali zake.
"Tungependa kuona na pengine kila wakati kusikia vijana mkiwa watetezi shupavu ambao mtakuwa mstari wa mbele katika kukitetea chama, sera zake pia mnaoijua na kuihifadhi siasa ya chama pia wenye nguvu za utetezi utokanao na nguvu ya hoja "alisema Balozi Mshangama.
Mwenyekiti huyo wa CCM pia alitoa wito kwa UVCCM kutenga wakati ili kutembelea wilaya ya Lushoto ambayo ni kubwa,yenye wakazi wengi lakini pia ni ngome ya ccm kabla na baada ya uhuru wa Tanganyika baadea ikaindwa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hata hivyo aliitaka jumuiya ya Vijana kuwa ya awali kuikosoa serikali kwa hoja kabla ya wapinzani hawajafanya hivyo kwasabahu kazi ya vijana ni kuelekeza , kukosoa na kusimamia yale yote yanayoonekana kwenda mzabwamzabwa au shagalabaghala Balozi huyo pia alitoa rai na kumtaka Kaimu Katibu Mkuu Shaka kuwasilisha kilio cha wananchi wa Lushoto mbele ya chama ambao wangependa siku moja kuona mkoa wa Tanga ukipatikana mkoa mwingine mpya kutokana na idadi kubwa ya wakaazi wake.
"Tuko wakaazi wengi ambao tunatosha kabisa kuwa na mkoa mpya pengine ungeitwa mkoa wa Usambara ,Lushoto ni sehemu yenye historia kubwa sasa na wakati uliopita, wana Lushoto tungefarijika sana jambo hilo litokee "alisisitiza mwanasiass huyo .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Uvccm mkoa wa Tanga alisema kwa hakika ukubwa wa mkoa wa Tanga inatosha kutoa mkoa mwingine mpya na kwamba wilaya hiyo kulingana na ukubwa wake inaweza hata kutoa wilaya mbili.
Kadhalika Makange alisema anaamini kuwa ombi hilo litashughuliiwa ipasavyo na mamlaka husika za utawala na kwanba siku moja ndoto hiyo inaweza kutimia.
"Mwenye kusubiri hachoki na mamabo mazuri hayataki haraka,iko siku jambo hili litakuwa na mkoa mwingie mpya utapatikana "alisems Makange.