Shaka
akiwa na ujumbe wake waliozuru katika kaburi la mwandishi gwiji wa
vitabu vya fasihi andishi na simulizi hayati Sheikh Shaaban Robert huku
mjinimwema mkoani Tanga
Na Woinde Shizza,Tanga
Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM) umesema utaieleza serikali mkoani Tanga kuondosha utata na mivutano iliopo katika kijiji cha mji mwema kati ya familia mbili husika mahali ambako amezikwa mwandishi bingwa wa vitabu vya fasihi simulizi na andishi Marehemu Sheikh Shaaban Robert.
Tamko hilo limetamkwa na Kaimu katibu Mkuu wa Uvccm Shaka Hamdu Shaka aliyefika katika kaburi la Mwandishi huyo galacha Afrika mashariki aliyezaliwa mwaka na kufariki mwaka 1962 .
Shaka mara baada ya kusafisha kaburi la marehemu na kuomba duwa akiwa na ujumbe wake alielezea na mjukuu wa marehemu Khatib Mwinjovu kwanba mahali hapo qlipozikwa sheikh Robert pamekuwa na mivutano isio na ulazima toka upande wa familia ya mke wa marehemu Robert.
Alisema kaburi hilo ni alama kuu katika Taifa letu hivyo halipaswi kuandamwa kwa mivutano au misuguano isio na sababu na kuahidi kwamba seeikali itatumia uwezo wake kuleta mapatano haraka.
"Nitaongea haraka na mkuu wa mkoa wa Tanga kuhusu utata huu, uvccm ingependa kuona kaburi la mwandishi huyo bingwa anayetajika duniani linatunzwa kwa heshima zote , ametumia maisha yake yote kuandika ili kuvielimisha vizazi na vizazi hadi sasa.
Aidha shaka aliitaka jamii kutambua na kuhshimu nguvu alizozitumia marehemu sahaaban katika uhai wake ambazo sasa alisema zinafaa katkka kizazi hadi kingine wakati yeye akiwa hana tija wala faida.
Kwa upande wake katibu wa ccm mkoa wa Tanga Shija Othman Shija alisema uamuzi wa UVVCM kuja kulizuru kaburi hilo ni tendo la kiungwana hivyo akatoa wito kwa jumuiya nyingine nazo kuiga mfano huo.
Shija alisema ni jambo lisilowezekana kuzungumzia nchi yetu kabla na hata baada ya uhuru bila kulitaja jina la marehemu Shaaban Robert kutokana na mchango wake mkubwa hasa katika mitaala ya elimu na ukuzaji lugha ya kiswahili.
"Robert amekuwa nguzo na kioo ambacho hakutavunjika wala kuingia nyufa wakati wote, maandiko yake yatabaki katika kurasa muhimu toka kizazi kimoja hadi kingine "alisems katibu huyo wa ccm mkoa.