Na Woinde Shizza,libeneke la kaskazini blog Arusha
Jeshi la
polisi mkoani Arusha linawashikilia watu 13 kwa kitendo cha kuuza sukari
kinyume na bei ilekezi iliyopangwa na serekali ya shilingi
1800.
Akiongea na
waandishi wa habari kamanda wa polisi
mkoa wa Arusha Charles Mkumbo Alisema
kuwa watu hao wamekamatwa katika maduka tofauti tofauti kufuatia operesheni
kabambe iliandaliwa na jeshi hilo kwa ajili ya wafanya biashara wote ambao
wanauza sukari bei ya juu pamoja na walioficha sukari .
Alisema
kuwa kumekuwa na wafanya biashara ambao
wamejipandishia bidhaa hii ya sukari na kuuza bei ambayo wanaitaka wenyewe
badala ya kuuza bei ambayo imepangwa na serekali ambayo ni shilling 1800.
‘kuna
wafanya bishara wameamua kujichukulia sheria mkononi na kuanza kuuza sukari bei
gali huku wengine wakiwa wanaficha sukari ili isiwepo madukani na wapandishe
bei jamba ambalo sio zuri ndugu waandishi tumewakamata wafanyabiashara 13 adi
sasa ambao walikuwa wamejipandishia bei kiolela olea na wengine wanauza sukari
adi shilingi 5500 kwa kili wengine 4500 huku wengine wakiwa wanauza 3000 kitu
ambacho sio cha haki na nikinyume na sheria “alisema Mkumbo.
Aidha
aliwataja baadhi ya wafanyabishara ambao wanashikiliwa na jeshi la polisi ni
pamoja na mmiliki wa Rafiki minisuper market
aliyejulikana kwa jina la Jemsi Wiliam ambaye yeye aliuza sukari kilo
moja kwa shilingi 5500,Pick pay supermarket ambeye yeye aliuza sukari kilimoja
kwa shilingi 3000,sayana Grokoli ambayo
inamilikiwa na Muhidin Kitibwi ambaye yeye aliuza sukari kilomoja kwa shilingi 5000 pamoja na mama Anna Silayo amabaye yeye
aliuza sukari kilimoja kwa shilingi 3000
huku Muhame Suhaul ambaye yeye alikuwa anauza sukari kilimoja kwa
shilingi 6200.
Alisema kuwa
watuhumiwa wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani na sheria itafata mkondo
wake na watashitakiwa kwa kosa la kuhujumu uchumi wa nchi..
Alitoa wito
kwa wananchi wa mkoa wa Arusha hususani ni wafanya biashara kuuza sukari kwa
bei elekezi iliotolew ana serekali na sio kujipandishia bei kiolela holela huku
akitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa mfanyabiashara
yeyote ambaye atakuwa anauza sukari kinyume na taratibu na Yule yeyote ambaye
atakuwa ameifadhi sukari nyingi katika gala au sehemu yeyote.
Mkumbo alimalizia
kwa kusema zoezi hili halitaishia hapa ni endelevu na wataendelea kufuatilia
kila kona kubaini watu ambao wanakiuka sheria.
Gazeti hili
lilibatika kuzungumza na baadhi ya wananchi wa jiji la Arusha nao waliomba
serekali iwafatilie wafanyabishara hawa wa maduka ambao wanauza sukari kwani
wanajipandishia bei kiolela hali ambayo inawafanya wanachi wengine kushindwa
kunywa chai asubui kutokana na kutoweza kununua sukari kwa bei ya juu