KESI YA UCHAGUZI LONGIDO SHAHIDI WA 19 NA 20 WATOA USHAHIDI






Shahidi wa 19 katika kesi ya uchaguzi Jimbo la Longido Mkoani Arusha,Lomayani Mollel{62] aliieleza mahakama jana kuwa alitoa taarifa kwa msimamizi wa uchaguzi kata ya Kamwanga kuwepo kwa majina ya wakenya kuwepoa katika daftari la wapiga kura katika kata hiyo.

Mollel alisema hayo mbele Jaji Mfawidhi kanda ya Bukoba,Silvangirwa Mwangesi anayesikiliza kesi hiyo wakati akihojiwa na wakili wa serikali Fortunatus Mhalila na wenzake Neema Mwanga na David Akway.

Amesema mbali ya kuwaona wakenya katika daftari hilo pia aliwashuhudia wakipiga kura katika kutuo cha madukani na wengine maeneo mengine kwani walikuwa na wino katika kidole ulionyesha kuwa walipiga kura siku ya uchaguzi octoba 25 mwaka jana.

Shahidi huyo aliulizwa na mwanasheria wa serikali Mhalila kuwa aliwajuwaje kama walikuwa wakenya alisema kuwa anawajuwa kwa kuwa ni majirani zake kwa upande wa Kenya na wao wanaishi upande wa Tanzania hivyo wanafahamiana vizuri.

Mollel alisema kutoka na utata huo wa wakenya kupiga kura nchini kinyume na uratatibu alitoa taarifa kwa msimamizi wa uchaguzi kata lakini hakuchukuwa hatua yoyote na pia alitoa taarifa kwa mgombea wa CCM,Dkt Stephen Kiruswa kuwepo kwa wakenya katika daftari la wapiga kura.

Shahidi huyo alisema kuwa yeye anajuwa kusoma na kuandika Kiswahili na kiapo alichokiwasiliha mahakamani  aliandika mwenye na kutafsiliwa kiingereza na wakili wake Edmund Ngemela na Daud Haraka.

Akihojiwa na wakili,John Materu aliulizwa ni watu gani wanapaswa kupiga kura,Mollel alisema ni watanzania wazalendo ndio wastahili kupiga kura na hajui kama wakenya hao walimpigia Dkt Kiruswa au la ila kitendo cha wao kupiga kilikiukwa.

Shahidi huyo aliulizwa ni kwa nini hakutoa taarifa kituo cha polisi Kamwanga wakati ni kosa la jinai,shahidi alisema jukumu lake lilikuwa kutoa taarifa kwa msimamizi wa uchaguzi wa kata tu na sio vbinginevyo.

Shahidi wa 20 katika kesi hiyo Isaya Mollel {43} mkazi wa kijiji cha Lalilangwa kata ya Olmoloko wilayani Longido yeye alisema mgombea wa Chadema Onesmo Ole Nangole alitumia lugha za kashfa katika mikutano ya kampeni iliyofanyika katika kata hiyo.

Alisema kashfa zilizotolewa na Nangole alizisikia mwenye katika mikutano mbalimbali ya kampeni na hajui kama mlalamikaji hajawasilisha katika malalamiko yake bali anajuwa alichoandika katika kiapo chake kilichosomwa mahakamani hapo.

Shahidi alikiri mahakamani hapo kuwa alimpigia kura ya ubunge Dkt Kiruswa lakini alisema alitaka mshindi ashinde kwa kufuata taratibu za uchaguzi.

Kesi hiyo inaendelea tena jumatatu mei 30 mwaka huu ambapo  mashahidi wa upande wa mlalamikaji wanatarajiwa kutoa ushahidi wao.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post