Na Woinde Shizza ,Arusha
Chama
cha wanunuzi na wauzaji wa Madini Tanzania TAMIDA kimetoa tamko la
kulaani kitendo cha uongozi wa Haliamshauri ya Simanjiro kuwavamia
wafanyabiashara wa madini wa jijini Arusha maofisini wakiwa
wameambatana na Askari wenye silaha za moto na pingu kuwalazimisha
kulipa kodi ya tozo ya huduma ya Madini.
Akitoa
tamko hilo katika mkutano wa wafanya biashara wa Madini uliofanyika
katika Ofisi za wizara ya madini Kanda ya Kaskazini jijini hapa Makamu
mwenyekiti wa TAMIDA Thomas Munis alisema kitendo hicho hakikubaliki na
kimelenga kuwadhalisha wafanyabiashara hao pamoja na wateja wao.
Thomas
aliutaka uongozi wa Wilaya ya Simanjiro kukaa chini na kukubaliana
namna ya ulipaji wa tozo hiyo inayofikia kiasi cha shilingi Milioni 20
hadi 60 kwa mwaka, jambo ambalo alisema hawawezi kulipa mara mbili kwa
halimashauri ya Arusha pamoja na Halimashauri ya Simanjioro.
"Sisi
kama wafanyabiashara hatupingi kulipa kodi yoyote ya madini ili tunacho
sikitishwa nacho ni hatua ya uongozi wa Simanjiro kutufuata maofisini
wakiwa na silaha za moto na pingu, kutaka tulipe kodi Huduma ambayo
kimsingi tumekuwa tukilipa kila mwaka katika halimashauri ya Arusha",
Alisema Thomas.
Aidha
aliongozea kusema kuwa wao kama wafanyabiashara wa madini hawapingi
kulipa kodi yoyote inayotozwa kutokana na biashara ya madini ila
wanachopinga kodi hiyo kutozwa mara mbili kwa mwaka katika halimashauri
zote swala ambalo wameliomba serekli kupitia wizara ya madini kuingilia
kati swala hilo na kutatua mkanganyiko huo.
Wakati
huo afisa madini kutoka ofisi hiyo ya kanda Bwana Erick Mpesa amesema
kuwa wao kama kama wasimamizi wa madini katika kanda hii wana ngoja
mafikiano ya pande zote mbili ikiwemo halimashauri ya Simanjiro pamoja
na jiji la Arusha juu ya Tozo hiyo ya huduma ya Madini.
Kwa
upande mwanasheria Jiji la Arusha Bahati chojo amesema kuwa sheria
inaelekeza wazi kuwa kampuni yoyote inayofanya bishara ya madini
inapaswa kulipa tozo ya huduma kule ilipo ikiwemo kulipa kule ilipo
ofisi pamoja na maeneo ya matawi ya ofisi hizo.