Ankal
Issa Michuzi anasikitika kutangaza kifo cha mwanae Maggid Muhidin
kilichotokea jana Jumapili huko Durban, Afrika Kusini, alikokuwa
masomoni.
Mipango
ya kuusafirisha mwili wa marehemu inafanywa, msiba utakuwa Tabata Mawenzi
jijini Dar es salaam ambako ratiba ya mazishi itatoka mara tu baada ya
mwili kuwasili.
Habari
ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale
walipo.
Innalillah wa inna ilayhi raajiun