BREAKING NEWS

Monday, May 9, 2016

BALOZI SEIF: MKITAKA ELIMU AU UJINGA MTAKUTANA NAO KWENYE KOMPYUTA


 
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi amesema ikiwa wanafunzi
wataitumia vyema mitandao ya kijamii kwa ajili ya kujenga ufahamu na
maarifa yao watafaidika na matumizi ya kompyuta na ikiwa wataamua kuusaka
ujinga watakutana nao kwenye matumizi ya teknolojia hiyo.
Amesema dunia ya sasa imekuwa ndogo kimawasiliano na upashanaji habari na
taarifa muhimu kutokana  na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa wepesi katika
kuitumia vyema teknolojia ya habari kwa usahihi bila kujingiza
katikqnupotoshaji au katika masuala mengine.
Balozi Seif ambaye pia ni Makamo wa pili wa Rais Zanzkbar  alieleza hayo
wakati akikagua madarasa ya Kompyuta ya Shule  za Sekondari za Kitope na
Mahonda katika Jimbo la Mahonda  mkoa wamkaskazoni Unguna mara baada ya
kupeleka  msaada wa vifaa hivyo na kuzindua rasmi madarasa yake.
Aidha msaada huo umezinufaisha takriban shule  hizo ikiwemo ile ya Kitope
iliokabidhiwa Kompyuta 25 na sekondari ya Mahonda ilipewa Kompyuta kumi.
Balozi Seif alisema mtandao wa teknolojia ya kisasa ya mawasiliano
imemsaidia  binaadamu kurahisisha maisha yake ya kawaida kwa kiwango
kikubwa kiasi kwamba taaluma hiyo pia imetoa fursa za ajira kwa vijana
wengi kwenye maeneo mbali mbali duniani.
Balozi Seif alisema  wimbo wa matumizi yq  sayansi na teknojia uliohanikiza
kila pembe ya dunia lazima kwa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla nwake
uelekee katika kusaidia kufanikisha na kutatua changamoto zinazoikabili
jamii  hasa watumishi wa taasisi za Umma na maendeleo ya nchi
Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mahonda pia  aliupongeza uongozi wa  Sekondari
ya Kitope kwa uamuzi wake wa kuanzisha darasa la Kompyuta litakalotoa fursa
kwa wanafunzi wake kuingia vyema ndani ya dunia ya utandawazi kwa kujiamini.
Akiguzisa changamoto nyingi zinazoikabili shule za Msingi na Sekondari
Mwakilishi huyo aliahidi kushirikiana na Wizara ya Elimu pamoja na Kamati
ya shule  katika kuangalia ni kwq kiwango kipi  changamoto hizo zinawe
kupungua kadri ya hali ya uwezeshaji

"¡nadhari shule za msingi na sekondari  zianze haraka kushirikiana pia
wazazi wa wanafunzi washiriiishwe katika kutafuta mbinu na kuweka mikakati
itakayosaidia kupunguza changamoto zilizomo katikauwezo wao"alisema
Aidha Balozi Seif aliwapa matumaini walimu na wanafunzi hasa wale wa shule
za msingi kwa kuwaahidi kutafuta wahisani watakaounga mkono nguvu ili
kusaidia madawati ya madarasa ya shule hiyo.
Alisema hatua ya kwanza itahusisha madawati  100 kati ya mahitaji halisi ya
madawati 300 tatizo ambalo limekuwa alikiziathiri shule nyingi za  Zanzibar
hata zile za  Bara.
" kutokana na upungufu wa madawati  baadhi ya viongozi wamebuni mbinu za
kuanzisha harambee ili kuzishirikisha taasisi na  mashirika ya maendeleo
kuchangia nguvu zao, tutafajya hivyo kwa maslani ya kizazi cha sasa na
kijacho "alisisitiza katika Katika risala iliosomwa Mwalimu Dadi Salum
Rashid  alimshukuru Mwakilishi huyo kwa jitihada zake za kusaidia
wanafunzi wa shule hiyo hatimae ifajye vyema katika mtihani yao
End

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates