SHAKA : MAALIM SEIF KIONGOZI KIHEREHERE NA PAPARA


  Mwandishi Wetu, Dodoma

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi umemtaja Katibu Mkuu wa Chama cha CUF seif sharif Hamad  ni mwanasiasa pekee  muflis miongoni mwa wanasiasa waliowahi kushiriki siasa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kwamba hakuna anayempita kiongozi huyo kwa sifa ya uzushi na ugombanishi .
Umoja huo umeeleza kuwa kiongozi huyo licha ya kutokubalika kwake ndani ya nchi yake pia amekuwa si kuongozi anayeaminika wala  kukubalika katika siasa za kitaifa na kikanda.

Matamshi haayo yametqmkwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka  wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa jumuiya hiyo toka ngazi za wilaya na Mikoa sita ya Kanda ya Kaskazini na Kati yaliofanyika mjini hapa.

Shaka alisema matamshi ya kiongozi huyo wa upinzani alidai kuwa Rais wa Seriiali ya Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein hatafika mwaka 2020 akiwa madarakani,aliziita  hizo ni njozi za  mchana anazoota kiongozi huyo ambaye sasa yuko katika juhudi ya kuwafariji na kuwapoza wafuasi wake.

Alisems Maaalim Seif hana ubavu wala ujanja wowote wa kumvuruga au kumuondoa Rais Dk Shein kwenye kitibchake na kwamba maneno hayo yabkiongizi huyo wa upinzani  si mapya kwani  hata mwaka 1995 alipochuana na Dk Salmin Amour akashindwa alitoa matamshi  ya sina hayo .

"Anayoyasema Maalim Seif ni maneno ya kitoto tunajua anachokitaka wala hakijikawahi kutokea mahali popote duniani, atausubiri sana urais ila hataukwaa milele, hana sifa wala viwango vya kuwa Rais wa Zanzibar "alisema shaka
Alisema UVCCM inamtambua kiongozi huyo ni kati ya vibaraka wachache  waliobaki Barani Afrika na mara zote huwa hafanani kimsimamo wala kifikra na baadhi wanasiasa  wenzake mashuhuri  wenye kuheshimika mbele ya jamii.
"Tanzania ni Taifa Huru, haliendeshwi kwa njozi au utabiri kwa kutegemea mataifa ya kigeni , mwambienin seif uchaguzi umekwisha na dunia iliwaona wananchi  wakipiga kura kumchagua Rais, mwakilishi na diwani huku yeye aiiwazuia wagombea wa chama chake"alieleza Shaka. 

Kaimu huyo katibu Mkuu wa UVCCM alisema Maalim Seif ana wajibu wa kutambua kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vikosi vya JWTZ havipo unguja na pemba ila vipo huko Tabora, Dar, Pwani , Iringa, Kagera , Mtwara na kwenginekovhivyo wanajeshi kuonekana  zanzibar si uchuro au muujiza.

Hata hivyo Shaka alisema wanajeshi wa JWTZ  wakiwa Zanzkabr hawakumpiga wala kumzuai mtu asioige kura au kumtisha yeyote , tunamtaka aache porojo na uongo wa kizamani , raia anayeigopa askari si  mwema ila ni mhalifu "alisisitiza 

Shaka alisema kwa watu wasiomjua Maalim Seif wafuatilie maisha yake katika siasa na hapo alidai ndipo watakappbaini kuwa amegombana na wanasiasa wengi mashuhuri akiwemo Mzee Aboud Jumbe,Sheikh Thabit Kombo, Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Rashid Kawawa na sheikh Idris Abdul Wakil.
"Vigogo wote wa siasa nchini amewahi kuhitakafiana nao kwa nyakati tofauti, hata Mwalimu Nyerere ambaye ndiye aliyembeba na kumfikisha daraja ya juu kisiasa alumshinda hatinaye akambwaga "alisema. 

Kiongozi huyo wa vijana alisema matamshi yake ni mambo ya kujifariji ambapo kimsingi hana mlango wala dirisha la kupita hadi amundoe Dk shein madarakani kabla ya mwaka 2020.

"Kama kweli Maalim Seif  anajiona  ameota  pembe, tunamtaka kwa porojo zake sasa aidhihirishie dunia, ajue tu smz iko pale madarakani kisheria na kikatiba , aendelee  kuwapiga drip huku akiwanusisha tumbaku wafuasi wake ila atahadhari sana kucheza na dola "alisema shaka

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post