Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WA KATA YA MABATINI JIJINI MWANZA WATAKIWA KUUNDA ZAIDI VIKUNDI VYA KIJAMII.

Diwani wa Kata ya Mabatini, Deus Mbehe, akizungumza katika uzinduzi wa Kikundi cha Ushirikiano People's cha Mabatini.

Wananchi wa Kata ya Mabatini Jijini Mwanza, wametakiwa kuunda na kusajili vikundi vya Kijamii kwa ajili ya kupata fursa ya kusaidiana katika shughuli mbalimbali ikiwemo maafa.

Diwani wa kata hiyo, Deus Lucas Mbehe (Chadema), alitoa rai hiyo juzi katika uzinduzi wa Kikundi cha kusaidiana cha Ushirikiano Peoples, kinachoundwa na wanachama wa Chadema kata ya Mabatini.

"Kupitia vikundi hivyo, wanajamii wataweza kusaidiana katika matatizo yanayojitokeza katika jamii ikiwemo misiba pamoja na kusaidiana kiuchumi kwa kutumia fursa zinazotolewa na serikali katika vikundi vya kijamii ambapo nawasihi msiingize ubaguzi wa aina yoyote ikiwemo udini na itikadi za kisiasa katika vikundi hivyo". Alisema Mbehe.

Abdallah Mkama ambae ni Katibu wa Kikundi cha Ushirikiano Peoples, aliwahimiza wananchi wa Kata ya Mabatini kujiunga na kikundi hicho ili kwa pamoja kuendeleza ushirikiano uliopo katika masuala mbalimbali ikiwemo starehe na maafa.

Kwa upande wake Salma Ibrahim ambae ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho, alitanabaisha kwamba  matarajio ya kikundi hicho ni kufanikiwa zaidi hususani katika kuinuana kiuchumi mbali na kusaidiana katika maafa na starehe.

Uzinduzi wa kikundi hicho chenye wanachama zaidi ya 100 uliambatana na harambee ya kukiimarisha kikundi ambapo zaidi ya shilingi milioni moja zilipatikana kwa ajili ya kusaidia utatuzi wa mapungufu yaliyopo ambayo ni ununuzi wa viti 120, sufuria nne, turubai mbili pamoja na sahani 200.

Post a Comment

0 Comments