Elizabeth Michael ‘Lulu’ akionyesha pete yake ya uchumba.
MSANII
maarufu wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibua gumzo kubwa
baada ya hivi karibuni kutinga kwenye Ukumbi wa Maisha Basement uliopo
Kijitonyama jijini Dar akiwa ametinga pete ya uchumba.
Lulu
akiwa ametinga kigauni chake kifupi cheupe alifikia kwenye ‘red carpet’
na kuanza kupigwa mapicha huku akiweka mapozi tofauti lakini kila pozi
alilokaa alihakikisha pete hiyo inaonekana. “Hee, huyu Lulu kavishwa
lini hii pete, na nani? Au ndiyo yule bosi wa redio?” alisikika akihoji
mmoja wa wadada waliokuwa eneo hilo na kuwafanya wengine waanze
kumjadili. Ndani ya ukumbi huo ilikuwa vigumu kuongea naye na
alipopigiwa simu ili azungumzie undani wa pete hiyo hakupokea