Na Woinde Shizza,Kilimanjaro
Jumuiya ya vijana UVCCM imetoa wiki moja kwa wale wote waliouza viwanja na rasilimali za jumuiya hiyo kujiandaa kwa ajili ya kupelekwa mahakani .
Agizo hilo limetolewa na kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka hamdu Shaka wakati akiongea na viongozi wa umoja huo wakiwemo wenyeviti wa mikoa ,wenyeviti wa wilaya pamoja na makatibu wa umoja huo kutoka katika mikoa ya Arusha ,kilimanjaro pamoja na manyara waliokutana katika ofisi ya CCM wilaya moshi mjini katika majumuisho ya ziara yake alikuwa akifanya katika mikoa hiyo.
Alisema kuwa baadhi ya watu wamegeuza mali za jumuiya hiyo kama shamba la bibi kwani kila mtu amaekuwa akitumia mali hizo na kuzitawanya kama anavyotaka hivyo ataakikisha anawachukulia hatua kali za kisheria kwa kuwapeleka mahakamani wale wote ambao wamehusika kufanya hivyo.
Alibainisha kuwa kwa sasa hivi katika uongozi wake amethamiria kuimarisha jumuiya hiyo ,na hata pepesa macho kwa yeyote yule wala kumuonea huruma yeyote yule ambaye amezifanya mali hizo za jumuiya kama shamba la bibi.
"nasema lazima nitampeleka mtu mahakamani ambaye atachezea mali za jumuiya kwani sasa ivi watu wengi wamegeuza jumuiya kama yao sasa nasema hivi nita kula nao sahani moja bila kuwaonea haya wala aibu tunataka kazi ambazo zinafanywa na jumuiya hii zionekana na watu wasione jumuiya hii kama mzigo ,tunataka kazi zinazofanywa na jumuiya zitambulike na tusiwe kama mzigo ndani ya chama sisi ni vijana tunanguvu ,uwezo tunao tukiamua kufanya kwa moyo na kwa nguvu zetu zote"Alisema Shaka.
Pia kwa upande wa utendaji ndani ya Jumuiya hiyo alisema kuwa kwa mtendaji yeyote ambaye anaona awezi kwenda na mabadiliko na kasi anayoitaka aachie ngazi mapema kabla ajamkuta maana atamuonea huruma yeyote kwani awataki watendaji wavivu wala mizigo ndani ya chama .
"napenda kusema kwa upande wa watendaji aijalishi wewe ni mwenyekiti ,katibu au hata katibu hamasa ukiona uwezi kuifanyia kazi chama achiangazi mapema tuandikie tuambie umeshindwa kazi dai mafao yako uondoke mapema kabla atujakukuta maana tukikukuta atuna cha salia mtume lazima tutakutoa narudia tena atutaki viongozi mizigo tunataka viongozi ambao wanafanya na wanafanya kitu kinachoonekana sio wanakaa tu ofisini kula kiyoyozi"alisema Shaka .
Alibainisha kuwa muda wa majungu ,fitina ,umbea na poroja umeisha na sasa ivi kinachoitajika ni mabadiliko ya utekelezaji wa majukumu ya kazi za kila siku kufuata vikao vya kikanuni na kubuni miradi ya maendeleo na itayokuza uchumi kwani UVCCM anayoitaji kwa sasa ni ya siasa na uchumi huku akiziagiza wilaya zote na mikoa kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo.
wabibi waliouthuria mkutano wa shaka w wakiwa wanateta jambo