Jana Alhamisi, Mei 19,2016 ilikuwa ni siku yenye furaha kubwa kwa Wanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza ambapo walikuwa wakisherehekea Mahafali yao ya Kuhitimu kidato cha sita.
Mahafali hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Shule hiyo, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni diwani wa Kata ya Mkolani Mhe.Dismas Rithe.