MAJALIWA : SEREKALI ITAHAKIKISHA INAENDELEA KULINDA RASILIMALI ZA NCHI IKIWEMO URITHI WA DUNIA


 
waziri wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa 

Woinde shizza,Arusha

SERIKALI ya awamu ya tano  imesema kuwa itaendeleza jitihada za
kutunza na kulinda urithi wa dunia ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi
wanaoishi maeneo ya uhifadhi ili watanzania wote waweze kunufaikana
rasilimali za nchi .


Hayo yalisemwa na  waziri mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akifungua
mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa afrika kama nyenzo ya maendeleo
endelevu unaoendelea mjini hapa.

Majaliwa alisema kuwa rasilimali zilizopo ni za watanzania na ili
kuhakikisha kuwa wananufaika nazoserikali itahakikisha  inatunza na
kulinda uhifadhi ili yawe endelevu na kuweza kusaidia vizazi vijavyo.

Alidai kuwa Tanzania ni moja ya tajiri wenye urithi na hivyo ili
kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika haswa waishio maeneo ya uhifadhi
serikali itatoa elimu ya kutosha ili waepuke kuchangia uharibifu
unaotokea kwenye hifadhi za taifa na hivyo kusababisha kuongezeka kwa
uchumi wa taifa na hata wananchi wenyewe.

 “rasilimali hizi ni zetu na hivyo hata wanaoishi maeneo ya hifadhi
watusaidie kwa wale wanaoingilia na kuharibu  kwani hata hizo mali
asili zinatusaidia sote na hata tumewekea mikakati ya kutunza maeneo
hayo ili yawe endelevu’alisema


Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo ambaye ni katibu mkuu wizara
ya mali asili na utalii meja jenerali Gaudence Milanzi Alisema kuwa
madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto na mambo ambayo
yanatishia  na kuadhiri uhifadhi bora wa maeneo ya urithi wa dunia
katika afrika .



Aidha mkutano huo utapendekeza suluisho kwa kupitia upya shughuli
zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango wa
miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi ijayo.

Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kushawishi
wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi inayoendana na uhifadhi
wa urithi na maendeleo endelevu pamoja kuchunguza jinsi mitafaruku
inayotokea kwenye maeneo urithi wa dunia  kutokana na makundi ya
kigaidi na kutunza amani utamaduni na uridhi asilia.


Aliongeza kuwa pia  mkutano huo umejikita kwenye sera ya UNESCO  ya
mwaka 2015 inayohusu kujumuisha maendeleo endelevu kwenye mkataba wa
uridhi wa dunia.

“mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa kisayansi, pia uatakuwa na
manufaa kwa taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kutalii na kisasa bali
pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi ya wageniwatakao
uthudhuria  mkutano huu pamoja na kuanzisha mitandao wa kitaaluma na
kujenga mataji wa kijamii”alisema Malinzi


Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote kutakuwa
na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa yakifanyika siku zote
za mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa katika hifadhi ya taifa
ya Ngorongoro

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post