Afisa usiano wa chama cha waajiri
(ATE) Patricia Chao akiwa anawapa maelekezo baadhi ya wateja wakigeni waliouthuria katika banda lao kujua jinsi ili kuweza kujua jinsi chama cha waajiri kinavyofanya kazi
Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi Gibson Olemeiseyeki akipata maelekezo ya huduma zinazotolewa na kampuni ya utalii OSUPUKO nature Paradise iliopo mkoani Arusha
Emma Saria Treasury Dealer wa benki ya ABC akiwa anawaonyesha wateja waliouthuria katika banda lao aina tofauti tofauti za kadi za benki zinazotolewa na banki yao
Meneja wa Banki ya ABC Joyce Malai akiwa anawapa maelezo ya huduma zinazopatikana katika benki yao na jinsi ya kufungua akaunti ndani ya benki yao ambapo alisema kuwa kima cha chini cha kufungulia akaunti ndani ya benki yao ni shilingi 5000 na benki yao inatoa huduma ndani ya nchi na nje kwani ni ya VISA na pia unaweza kulipia kitu chochote ukiwa na kadi yao ATM card
meneja wa Banki ya Banc ABC yenye tawi lake Arusha karibu na hospitali ya ST.Thomasi Mbuche Zambi akiwa anaongea na wateja (hawapo katika picha) waliouthuria banda hilo
wananchi wakiendelea kupata maelezo ya utalii ndani ya banda la Ngorongoro Conservation lililopondani ya maonyesho hayo
kikundi cha ngoma kikiendelea kutumbuiza
wamama wa kimasai wakiwa wamekaa wanaangalia burudani mbalimbali za vikundi vya ngoma
kikundi cha ngoma kutoka morogoro kikiendelea kutumbuiza ndani ya baadhi ya mabanda yalikuwepo katika maonyesho |
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Serikali imetakiwa kufungua ofisi za utalii katika
kila nchi ambazo zinaleta watalii hapa
nchini pamoja na kupunguza viingilio vya wageni wanaotembelea hifadhi zetu za
taifa ili kuweza kuongeza idadi ya watalii wanaoingia hapa nchini .
Hayo
yamebainishwa na mbunge Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi Gibson Olemeiseyeki wakati alikuwa akiongea na
waandishi wa habari alipotembelea katika maonyesho ya utalii ya Karibu fair
yanayofanyika ndani ya viwanja ya magereza nje vilivyopo ndani ya jiji la
Arusha .
Alisema
kuwa serekali inapaswa kufungua ofisi
katika kila nchi ambayo inajua
inaletawageni hapa nchini ili kuweza kutangaza utalii wetu vizuri,na ili kuweza
kupata wageni wengi zaidi ambapo
wakiingia kwa wingi watasaidia kuongeza pato la taifa na kupunguza tatizo la
ajira kwani vijana wengi wanaweza kujiajiri kupitia utalii pamoja na biashara
za utalii .
Alibainisha
kuwa ni jambo la ajabu nchi kama Tanzania
ambayo inavivutio vingi vya utalii huku
ikiwa ni nchi mojawapo ambayo iko katika
nchi kumi bora ambazo zinaongoza kwa kuwa na vivutio vya utalii lakini ni nchi
ambayo inaongiza watalii wachache sana ukilinganisha na vivutio vilivyopo.
“nchi
kama Tanzania pamoja na vivutio vyote
lakini kwa mwaka tunaingiza watalii milioni moja wakati nchi kama maleshia kwa mwaka
wanaingiza watalii miolini 15 ni jambo la kushangaza alafu ukiwaangalia
viongozi wetu badala ya kukaa na kuangalia jinsi ya kufanya ili wataliii wangie
na wawe wengi lakini wao wanakaa wanachekelea na wanafanyakazi ya kuongeza ada
ya kuingia katika ifadhi yetu kila mara sasa hiii kweli si itakimbiza wageni
badala ya kufanya wageni waongezeke kila siku”alisema Olemeiseyeki
Alisema
kuwa kupitia utalii serekali inaweza kuingiza ela nyingi sana na sio ola pia
inaweza kuwaachiri vijana wengi sana
,iwapo ikijipanga vizuri na kutumia fursa vizuri kwani kama nchi
zingine zinaweza ata serekali yetu itaweza iwapo tu itaajiri wafanyakazi ambao
wanauchungu na hifadhi zetu na pia wanataaluma ya kutosha kuhusiana na utalii
na sio kuajiri watu ambao awana taaluma na kuajiri watu kiundugu undugu na
kiubinamu.
“unajua
ukiona bidhaa aina soko unatakiwa uishushe bei na uangalie nini cha kuboresha
ili uweze kuuza bidhaa yako sasa apa kwetu viongozi wanapandisha bei kila siku
awaangalii ni chakufanya ili utalii na watalii waje kwa kasi hapa nchini badala
yake wanapandishi kila kitu sasa kibaya zaidi ata bei za ndege ambazo zinaleta
wazungu zikitaka kutua hapa kuleta watalii yaani wanapangiwa garama kubwa mno
kiasi kwamba wanashindwa kuja inabidi waende katika nchi jirani ya Kenya wakatue
maana wenzetu wanatambua umuimu wa kushusha bei na ukiangalia sasa ivi pamoja
sisi tuna vivutio vingilakini nchi ya Kenya inajulikana kuliko nchi yetu Tanzania
ambayo inavivutio “alisema Olemeiseyeki
Aidha
alimalizia kwa kuitaka serekali kupunguza tozo za utaliii pamoja na kuraisisha
ujaji wa wageni hapa nchini ili kuweza kukuza ongezeko la watalii hapa pamoja
na kuboresha miundo mbinu ndani ya hifadhi zetu.
Kwa
upande afisa usiano wa chama cha waajiri
(ATE) Patricia Chao alisema kuwa maonyesho ni mazuri na
kwani muamuko upo kwani watu wameuthuria tofauti na kipindi kingine kwani amewaona washiriki wengi kutoka nchi
mbalimbali ikiwemo kenya ,uganda ,Rwanda ,Burundi na hata South Afrika tofauti
na kipindi kingine.
“kiukweli
maonyesho ni mazuri lakini pia naisi ukosefu wa fedha ndio umefanya pia
wamiliki wengi wa utalii kutokuja kuonyesha bidhaa zao kwa sababu nyie wenyewe
waaandishi mmeona hamda kampuni kama Leopard tours ,sopa lorge pamoja na serena
hii inaonyesha ni jinsi gani sasa ivi hela hamna na ukiangalia garama pia ya
kuwa na banda hapa ni kubwa sana sasa mtu akiangalia anaona kuliko apoteze
fedha yake bure ni bora asije kuonyesha kwakweli napenda kutumia mda huu
kuwasihi waandaaji wa maonyesho haya kupunguza garama za kuwanabanda hapa
pamoja na hata ya kiingilio siku ya kwanza ili kila mmoja awe ze kuja na
kujionea “alisema Afisa biashara wa Serena hotel Jonathan Njotto.