Wadau wa Mawasiliano Kanda ya Ziwa, wakiwa katika picha ya
pamoja katika Semina juu ya utoaji wa elimu juu ya simu bandia (fake) na halali
(orginal) ulioandaliwa na TCRA, kabla ya kusitisha matumizi ya simu bandia
mwezi ujao.
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imeendelea
kuwakumbusha watumiaji wa simu za mkononi kuhakiki simu zao kabla mamlaka hiyo
haijazima simu bandia ifikapo Juni 16 mwaka huu.