Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Mkoani Arusha (UWT) Flora Lazaro Zelothe.
Katibu wa Jumuiya wa wanawake Tanzania Mkoa wa Arusha (UWT) Bi Fatma Tsea.
Katibu wa CCCM Wilaya ya Arusha Mjini Ndugu Feruz Bano (ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo)
Mjumbe anayewakilisha Wazazi katika Jumuiya ya Wanawake Arusha (UWT) Phidesia Mwakitalima akifatilia uchaguzi kwa makini .
UWT.Wilaya ya Arusha Mjini wakiwa katika ukumbi wa CCM mkoa wakisubiria kumchagua Mwenyekitiwa UWT Wilaya
Umoja
wa wanawake Tanzania Mkoa wa Arusha Wilaya ya Arusha mjini wamefanya
uchaguzi ili kumpata mwenyekiti wa (UWT)katika wilaya hiyo.
Mwenyekiti
wa (UWT) Mkoani hapa Flora Lazaro Zelothe, amesema kuwa lengo la
uchaguzi huo ni kumpata mwenyeketi wa umoja wa wanawake Wilaya ya Arusha
mjini na kuongeza kuwa watu wenye maslahi binafsi hawawahitaji bali
watu wenye mapenzi mema na umoja huo.
Flora amewataka wanawake kuacha makundi kwani yamekuwa yakiwatenganisha
na hayana faida yeyote zaidi yakubomoa ,Bali wafanye kazi kwa bidii
nakujituma kwa kushirikiana na viongozi wao,ili kuleta mafanikio
katikaumoja huo.
Mary Kissaka baada ya kuchaguliwa kuwa.
mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Arusha Mjini.
Baada
ya kutangangazwa kuwa mshindi kwa kura 319, Bi Mary Kissaka
amewashukuru wanawake kwa kumchagua kwa kumpa kura za heshma,na ameahidi
kwamba atawatumikia UWT.Kuanzia ngazi Tawi, Kata ,hadi Wilaya kwa
kushirikiana na wanawake.
Ameongeza
kuwa Aatafanya ziara kila tawi ,ili kufanya tathmini ya uhai ya
wanachama, ili kila mwanachamaaweze kulipa ada ya mwaka kwa wakati, Pia
amesema kwa ataanzisha miradi mbalimbali kwa kushirikiana na UWT.
Sambamba
na hilo amewashauri wanawake wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi zinapojitokeza kwani wanaweza, na amewataka kuzitumia nafasi
hizo vizuri ili kuleta maendeleo katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Shabani Mdoe Katibu Mwenezi Uvccm Arusha naye alialikwa katika uchaguzi huo akiteta jambo.
Viongozi
wa CCM wilaya ya Arusha wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wilaya ya
Arusha Mjini Ndugu Wilfred Soilel, anayefuata ni Ndugu Feruz Bano ambaye
ni Katibu Katibu wa chama wilaya
Wanawake wakishangilia baada ya kumpata mwenyekiti wa kuiongoza UWT Wilaya ya Arusha Mjini.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha