Rais Magufuli ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara walioficha sukari ili baadae waiuze kwa bei kubwa.
Amesema
wafanyabiashara hao wenye tamaa ya pesa walikuwa wakifuata sukari iliyo
Expire huko Brazili na kuileta nchini ili watengeneze faida na ndo
maana serikali iliwapiga marufuku kuagiza
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiwasalimia wananchi wa Katesh,
Mkoani Manyara. Rais ametoka Mkoani Dodoma leo, anaelekea Mkoani Arusha
kwa usafiri wa gari.
Akiongea
na mamia ya wananchi hao waliojitokeza kumlaki njiani, Rais Magufuli
amewatoa hofu wananchi kuhusu uhaba wa sukari kwa kuwa tayari wako
katika mchakato wa kuagiza makontena ya sukari nje ya nchi ili
kuwakabili wafanyabiashara walioficha bidhaa hiyo.
Amesema
kwa taarifa alizonazo kuna mfanyabiashara alienda akanunua sukari pale
Kilombero zaid ya tani 3000 na hataki kuzichukua hadi leo
Pia amesema kuna mwingine ana godauni huko Mbagala yenye tani 4000 ambazo hataki kuzitoa ili wananchi wakose sukari