Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Francis Miti.
Na Woinde Shizza,Monduli
Imeelezwa kuwa Asilimia
10 ya watoto wilayani Monduli wanatajwa kutokwenda shule kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo utoro,pamoja na kufanya biashara katika baadhi ya minada wilayani humo jambo ambalo
limeamsha hisia za viongozi wa wilaya na kuamua kufanya operesheni ya
kuwakamata na kuwapeleka shule kwa lazima Zaidi ya watoto 21.
Hayo
yameelezwa leo naAfisa elimu msingi Theresia Kyala kutoka wilaya ya
Monduli mara baada ya ya zoezi la ukamataji wa watoto watoro amnao
wanafanya biashara eneo la minada ambapo zoezi hilo lilifanyika mnada wa
katika eneo la losirwa iliyoko kata ya mto wa mbu iko ambapo ni
utekelezaji wa agizo la Mkuu wa wilaya ya Monduli bw,Francis Miti ambapo
eneo hilo lina wakazi laki tatu kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 huku
Zaidi wakiwa
ni wakazi wa jamii ya kifugaji.
Ambapo
zoezi hilo limeendeshwa chininya usisamizi wa mkuu huyo na uongozi wa
idara ya elimu imetembelea eneo la mnada wa Kigongoni na kuona watoto
namna
ambavyo wanaendelea kufanya biashara ndani ya mnada huo wakati wenzao
wakiwa
madarasani ambapo nikazungumza na baadhi ya watoto hao ambao wanaelezea
baadhi
ya sababu zilizowapelekea kutokwenda shule ikiwemo ugumu wa maisha huku
wengine
wakishindwa kujielezea.
Theresia
Kyara
ni afisa elimu msingi wilayani Monduli alisema kuwazoezi la
operesheni hiyo
wameianza rasmi katika soko la Alhamisi la eneo la monduli mjini na
kufanikiwa kukamata watoto 16 na leo
hii wamekamata watoto 21 hii kati ya hao watoto sita wamepelekwa bweni
shule ya Manyara inaongeza idadi ya watoto ambao hawajaenda shule
katika wilaya hiyo.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya hiyo ya Monduli Francis Miti amesema kuwa
ameamua kutoa agizo hilo na kutekelezwa kwa lengo la kuwawezesha kwa
kila mtoto mwenye sifa ya kwenda shule aweze kupata elimu hiyo ya
kuanzaia msingi bure kwa lengo la kumuunga mkono mh,Rais katika utoaji
wa elimu bure ili kuweza kuweza kushinda katika sekta ya elimu.
Pia
amewataka wazazi wote wenye watoto kuhakikisha wanapeleka shule watoto
wao na kuwaandikisha na endapo mzazi ama mlezi atakae mhusisha na
kumkataza mtoto wake hatua za kisheria zitachukuliwa.
Mkuu
wa wilaya ya Monduli ameongeza kuwa zoezi hili la ukamatwaji wa watoto
hao ambao kati yao wapo waliotoka kwaajili ya kuchunga katika minada
huku wengine wakiwa hawajasoma kabisaa.
Nae mmoja wa mzazi bi,Moses ole laizer amesema kuwa zoezi hilo la kukamata watoto hao litaleta tija katika
jamii kutokana na kuwa hakuna sababu inayofanya watoto hao wasiende shule
kutokana na elimu kuwa bure na wazazi kuwaachia baadhi yao kuenda kufanya biashara minadani.
Aliongeza kuwa baadhi ya Jamii za kifugaji hususani wamasai wamekuwa na muamko mdogo wa
kupeleka watoto wao kupata elimu jambo ambalo linawanyima haki ya msingi kwa
kila mtoto mwenye sifa kwenda shule
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia